Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Dola sifuri ifikie mwisho Tabora’

Mkuu wa wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora akimuwakilisha mkuu wa mkoa huo hapa anazungumza na wakulima wa Tumbaku mkoa wa Tabora katika hafla ya jukwaa la pili la maendeleo ya ushirika mkoa wa Tabora lililofanyika katika ukumbi wa CCM wilayani humo. Picha na Hawa Kimwaga.

Muktasari:

  • Katika mauzo ya tumbaku kuna wakati inaweza kuuzwa kwa dola sifuri ambayo ni sawa na Tumbaku ya Kg1 inauzwa kwa Sh1,000 au Sh800 jambo ambalo wakulima wamelilalamikia kuwa linachangia hasara kubwa.
no

Tabora. Wakulima wa tumbaku mkoani Tabora wameelezea malalamiko yao kuhusu bei ya ‘dola sifuri’ katika mauzo ya zao hilo, hali inayowasababishia hasara kubwa. 

Wanasema iwapo tumbaku itaendelea kuuzwa kwa Sh800 hadi Sh1,000 kwa kilo moja, wataendelea kupata hasara.
Akizungumza leo Mei 11, 2025, wakati wa hafla ya jukwaa la pili la maendeleo ya ushirika mkoani Tabora lililofanyika ukumbi wa CCM, wilayani Nzega, Katibu wa Jukwaa hilo, Nassoro Mwandele amesema bei ya dola sifuri inawadhalilisha wakulima.

“Ni kweli inaweza kuwa tumbaku haina ubora, lakini mnunuzi huinunua kwa bei ya chini mno. Lakini akiipeleka kwenye masoko makubwa, huuzwa kwa bei ya juu, mkulima anaambulia kidogo, hali inayoonyesha kuwa tatizo si ubora pekee,” amesema Mwandele.

Mrajisi msaidizi wa sekta ya uhamasishaji, Ibrahim Kadudu, akimuwakilisha Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, amesema Sh58 bilioni tayari zimewekwa katika akaunti ya benki ya ushirika kama mtaji na kati ya hizo, Sh10 bilioni zilitolewa na Serikali kama sehemu ya kuimarisha taasisi hiyo muhimu kwa wakulima.

“Rais ametambua mchango wa mkulima na ameongeza nguvu kubwa. Tunatoa wito benki hii itumike kikamilifu kuwasaidia wakulima,” amesema Kadudu.

Kwa upande wake, Mkaguzi kutoka Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), Justine Maro amesema vyama vya ushirika 490 vimekaguliwa hadi sasa na vyama vinne tu vilivyopata hati safi. 

Wakulima wa Tumbaku mkoa wa Tabora wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Nzega katika hafla ya jukwaa la pili la maendeleo ya ushirika mkoa wa Tabora lililofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Nzega. Picha na Hawa Kimwaga

Vyama 380 vilipata hati zenye mashaka, 82 hati chafu, na 24 zilipata hati zisizo na maoni.
Amesema hali hiyo ni matokeo ya kutozingatia utunzaji wa kumbukumbu muhimu katika vyama hivyo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Saidi Nkumba ametoa onyo kali kwa watendaji wanaokwamisha malipo ya mbolea ya ruzuku kwa wakulima, akisema ifikapo Jumanne, Mei 13, 2025, endapo bado kutakuwa na wakulima ambao hawajalipwa, basi chama kitachukua hatua kali dhidi ya wahusika.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai amewataka wakulima kuacha kudanganywa na walanguzi wa tumbaku na kukemea tabia ya usafirishaji haramu wa zao hilo.

"Tumieni benki yenu ya ushirika. Rais amewekeza fedha nyingi kwa ajili yenu. Pia, wekeni msimamo mkali dhidi ya walanguzi na watoroshaji wa tumbaku kwani wanawakwamisha kwenye mafanikio," amesema Tukai.