Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema Sepetu apotezea ishu ya fomu, akomaa na Whozu

Muktasari:

  • Lakini, Dakika 5 zilitosha kupiga stori na Wema ili kufahamu kama atachukua fomu au vipi na pia kuhusu mahusiano yake na msanii wa Bongofleva, Whozu.

Dar es Salaam. Ikiwa  mashabiki wengi wa burudani na mitindo wakimsubiri aende kuchukua fomu ya kuwania kuomba uteuzi wa chama cha siasa kwa ajili ya kuwa mwakilishi wa wananchi kama walivyofanya baadhi ya wasanii. Wema Sepetu yupo bize na mambo mengine akiwa hana mpango wa kuchukua fomu, na hii ni kutokana na hofu baada ya kushindwa kwenye kura za maoni alipowahi kugombea ubunge wa viti maalumu kule Singida mwaka 2015.

Lakini, Dakika 5 zilitosha kupiga stori na Wema ili kufahamu kama atachukua fomu au vipi na pia kuhusu mahusiano yake na msanii wa Bongofleva, Whozu.

Mwananchi: Habari, sikupati vizuri simu inakoroma sana, uko wapi?

Wema: Niko Shinyanga kwenye kampeni yangu ya ‘Wema wa Mama’.

Mwananchi: Vipi kuchukua fomu wewe maana naona wasanii wengi safari hii wamejitokeza kuchukua. Je huutaki tena ubunge wa viti maalumu?

Wema: Mimi sina jibu sahihi kwa sasa maana nipo bize na hii kampeni niliyoianzisha. Pia niwape tu hongera zao wasanii wenzangu kwa kupata mwamko zaidi wa kuchukua fomu, kila la heri kwao.


Mwananchi: Vipi upo na Whozu kwenye hiyo kampeni?

Wema: Hapana sipo naye, niko na timu yangu tu Whozu yuko Dar es Salaam.


Mwananchi: Au ndio kweli mmeachana, penzi limekufa? Maana mara nyingi hupenda kuongozana, sasa imekuwaje umemuacha?

Wema: Whozu ana majukumu yake mengine na hata kama akija huwa hakai sana anarudi Dar sababu mimi hii kampeni nazunguka mikoa mingi sasa kuwa naye huko kote mambo yake yatalala.

Na kuhusu kuachana labda leo niseme kitu kimoja, mimi siwezi achana na Whozu sababu tunasikizana sana kwa mazungumzo na pia ndoto zetu za kimaisha zinaambatana, hivyo kugombana ni kitu cha kawaida na huwa tunawekana sawa.


Mwananchi: Mara nyingi mastaa huwa hawadumu na wapenzi na hata wewe hiyo tabia uko nayo, lakini Whozu wewe mpaka sasa mna takribani miaka mitano na miezi unaweza kutuambia siri ni nini?

Wema: Kikubwa ni kuzungumza na moyo wako ulipotua ni mahali sahihi na je, unapata faraja unapokuwa hapo? Mi’ na Whozu tunasikiliza sana.


Mwananchi: Ni kitu gani ulikipenda kwa Whozu?

Wema: Unajua napenda sana mwanaume asiyekuwa na kero, asiyependa kuzungumza sana yaani kiufupi sipendi gubu. Sasa kwa Whozu vitu vyote hivyo hana na huwa napenda sana anavyonichekesha nikiwa naye huwa nacheka sana.

Mwananchi: Ulishawahi kupigwa hata kofi na Whozu?

Wema: Siyo kofi tu tunapigana kabisa, lakini baadaye kama akigundua kama alinipiga kwa hasira basi anajirudi tunaombana msamaha na maisha yanaendelea.


Mwananchi: Ulishawahi kumfumania au yeye kukufumania?

Wema: Nilishawahi kumfumania mara nyingi, na yeye alishawahi kubamba meseji kwenye simu yangu, lakini inaonyesha labda mtu alikuwa ananipenda na mimi nikampotezea na ishu kama hiyo ya kufumania ni lazima itokee hasa kwa sisi ambao tuna majina.


Mwananchi: Kwa kipindi ambacho upo na Whozu hakuna ushawishi uliwahi kupata kutoka kwa mapedeshee mbalimbali?

Wema: Hata kama wapo sasa hivi siwezi kurubunika kwa sababu hakuna gari ambalo sijaendesha, viwanja ambavyo sijaenda na hela gani ambayo sijashika, hivyo mwisho wa siku unaona yote ni mapito tu.

Mwananchi: Whozu umemzidi miaka mingapi?

Wema: Nimemzidi miaka sita ambayo kwangu naona sio mibaya sana hata kama ingekuwa 15 kwani shida iko wapi?


Mwananchi: Penzi lenu lina changamoto?

Wema: Ndio sababu watu wengi kwanza hawakuamini kama nitakuwa na Whozu, na baadhi yao walisema sana na kunidhihaki, lakini mwisho wa siku mimi ndio mhusika nimependa iwe hivyo.