Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema atoa uamuzi wa mwisho wasioamini kujifungua kwake

Muktasari:

  • Mwigizaji huo ameeleza kuwa kwa sasa hatoendelea tena kusikiliza maneno ya watu kwani yanapoelekea yatamkata maziwa. Na kusababisha mwanaye akose chakula.

Dar es Salaam. Mwigizaji na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu ametoa uamuzi wa mwisho kuhusu baadhi ya watu wanaodai ujauzito wake sio wa kweli badala yake alivaa tumbo la bandia.

Mwigizaji huyo ameeleza kuwa kwa sasa hatoendelea tena kusikiliza maneno ya watu kwani yanapoelekea yatamkata maziwa. Na kusababisha mwanaye akose chakula.

"Uamuziki wa mwisho sasa sikilizeni nyie watesi sijui vitu gani? Siwezi endelea kuwapa proof kwa kitu ambacho hata nikifanya nini mtabaki kuwa negative. Maana naelewa nimewapiga na kitu kizito. 

"Inshort hamkutegemea kama ingekuwa hivi. Suprise haters kwahiyo endeleeni tu kuwaza mnavyojua. Kwa sababu nimeshaona nikiwaendekeza nyie mtakuja nikata development ya maziwa yangu bure nikamkosesha mwanangu chakula,"ameeleza Wema

Hata hivyo mwigizaji huyo ameeleza kuwa kwasasa anaenda mapumziko ya kutumia mitandao ya kijamii, hadi 40 ya mwanaye itakapofika.

"Naenda break off social media tutakutana 40 ya Baby Ollie. Nafunga hii chapter ya kuprove kitu ambacho hata mfanye nini ndiyo kishakuwa.

"Mungu amenipendelea ndiyo mjue hivyo, hayo yenu bakini nayo wenyewe. Hayanihusu, i have better things to do. The most important thing right now is My Baby Ollie,"ameeleza Wema 

Utakumbuka Wema na mpenzi wake Whozu walibahatika kupata mtoto wa kiume Juni 12,2026. Mtoto huyo anafahamika kwa jina la Ollie