Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utamu wa miss Tanzania ulimalizwa hapa

Muktasari:

  • Wote ni maarufu. Lakini ni Wema aliyekuwa na umaarufu ambao hata watu maarufu walitamani kuwa yeye. Alipendwa na wengi waliompenda walimpenda bila sababu. Dunia hii wapo wengi wanaopendwa bila sababu kama Wema.

Dar es Salaam, Bado mwaka mmoja tu, Miss TZ wa 2006 watimize miaka 20. Wema Sepetu (1), Jokate Mwegelo (2), Lisa Jensen (3), Sarah Kangezi (4), Irene Uwoya (5). Kuna Aunty Ezekiel na Malika Designer waliokuwa nje ya 5 bora.

                       

Wote ni maarufu. Lakini ni Wema aliyekuwa na umaarufu ambao hata watu maarufu walitamani kuwa yeye. Alipendwa na wengi waliompenda walimpenda bila sababu. Dunia hii wapo wengi wanaopendwa bila sababu kama Wema.

Wema. Ana mamilioni ya wafuasi ambao wanampenda kwa maana ya kumpenda. Lakini sababu ya kumpenda hawana. Ila wanampenda. Ni kipawa. Karama ya kupendwa tu na watu. Hana filamu wala tamthiliya Azam. Lakini yupo kwenye ‘meinistrimu’.

Hana uwezo wa kuigiza kumzidi Kemmy, Mona, Lulu na Johari ila anapendwa zaidi. Hana urembo kuwazidi washiriki wote wa Miss TZ 2006. Lakini watu walimpenda zaidi Wema kuliko washiriki wenzake. Aliendelea kuwa staa mkubwa bila taji.

                     

Kuna mamilioni ya roho zinazomfuatilia mitandaoni. Maelfu kama siyo malaki na mamilioni ya watu wanaotaka kujua chochote kuhusu Wema.

Hahitaji kubeba unga ili awe milionea. Wala kubeba bahasha na kuingia katika maofisi kuomba ajira. Wema siyo wa kusaka namba za maofisa masoko wa makampuni kuomba ‘dilizi’. Wao ndiyo walipaswa kumsaka Wema ili waingize pesa.

                       

Kuna mabinti hukaa vyumbani wakiwa watupu na laptop au simu. Kazi ni ‘kukommenti’ katika ‘peji’ ya Wema. Nao wanapata mashabiki na wateja wengi. Wapo wanaoandika mabaya tu. Nao wanapata mashabiki kwa sababu baya au zuri la Wema hufuatiliwa sana.

Kazi rahisi zaidi ni kutengeneza pesa kupitia jina la Wema. Lips zake ni pesa. Hips zake ni pesa. Nywele zake ni pesa. Kope za Wema ni utajiri. Jina lake ni pesa. Hata kumuhoji juu ya uhusiano wake wa mapenzi ni pesa. Tangu na tangu. Hakuna mwaka ambao Miss TZ ilitengeneza mastaa wengi kama 2006. Ndiyo mwaka ambao mpaka mshiriki aliyekuwa nje ya 10 bora naye akawa staa mkubwa.

Miaka iliyofuata halikuwa shindano la kumpata Miss Tanzania. Bali zilikuwa ni tafrija za kumnasa Miss Tanzania. Kutafuta msichana wa kuwakilisha nchi kwenye Miss World. Kila kitu kulienda kombo.

                     

Washiriki walishiriki ili wawe kama Wema Sepetu na siyo wawe Miss Tanzania. Hata waandaaji wa mikoani na vitongojini waliandaa ili wapate pesa za pombe na siyo wawakilishi bora.

Hata ngazi ya taifa huko, shindano liliandaliwa kama vile mtoto yatima. Halikuwa na mashiko tena. Mapedeshee wakateka kila kitu. Na kugeuza kama shindano la kupata totozi za kula nazo bata mjini.

Msichana wa pedeshee mwenye pesa akawa na nafasi ya kushinda. Bila kujali uwezo wa kujieleza kwa lugha au ushawishi. Hapo ikazidi kuharibika zaidi. Na pisi zikaanza kuona sehemu sahihi ni kwenye filamu.

Baada ya kuona dada zao wenye mataji ya Miss TZ wanahamia kwenye filamu. Kila Miss akataka kuwa muigizaji. Anko Lunde naye akalitema. Hakuna aliyetamani kuwa Flaviana wala Magesse.

Akili ya miss ilijielekeza zaidi Bongo Movie na Bongo Fleva badala ya mitindo. Kabla ya kina Wema Sepetu, ilikuwa fahari sana familia kutoa binti akawa Miss TZ. Ila baadaye ikawa fedheha kwa familia binti akishiriki Miss TZ.

Waandaaji wakaanza kukosa warembo wenye viwango. Waliogopa kudhalilisha familia kwa kushiriki kitu kisicho na sifa njema. Shindano likakosa mvuto kwa warembo wenye mvuto.

Na likakosa mvuto kwa mashabiki. Kisha likakosa mvuto kwa wadhaamini. Habari ikaishia hapo. ‘Anko’ Lunde kupitia wazo lake la Miss TZ kalizalisha mastaa wengi wa kike.

Ambao kupitia Miss TZ  maisha yao yalibadilika kabisa. Aina ya warembo walioshiriki miaka ile ilifanya shindano liwe na hadhi kubwa. Baada ya ushindi wa Wema 2006. Kilibadilika kila kitu. Lakini kwa sasa hata wao. Yaani Ma-miss TZ wa 2006, siyo mamisi tena. Kila kitu kimebadilika mpaka aina ya shughuli zao.