Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukistaajabu ya Jux utayaona ya Darassa na Marioo

Muktasari:

  • Kila mtandao wa kijamii unaoingia, ilikuwa ni picha za mastaa wa Bongo wakiwa harusini pamoja na hashtag ya #JP2025. Wengine hadi walikuwa wanatengeneza ‘meme’ wanasema, “leo bora ukose kula lakini sio bando

Dar es Salaam. Umeona jinsi juzi mitandao ya kijamii ilivyochafuliwa na harusi ya Jux iliyofanyika huko Nigeria? Sio Instagram, Tiktok, X wala Facebook.

Kila mtandao wa kijamii unaoingia, ilikuwa ni picha za mastaa wa Bongo wakiwa harusini pamoja na hashtag ya #JP2025. Wengine hadi walikuwa wanatengeneza ‘meme’ wanasema, “leo bora ukose kula lakini sio bando.

"Kwenye uwanja wa komenti wa kila posti inayohusu harusi hiyo ilikuwa ni kama uwanja wa vita. Watu wanatupiana makombora sio poa.

Wengine wanasema Wabongo hawajapendeza huku baadhi wakijibu ungeenda wewe unayejua kupendeza tuone. Wengine wanasema badala ya Wabongo kuvaa Kinaijeria wangevaa Kimasai kuwakilisha taifa ilhali wengine wanajibu “utavaa kimasai kwenye harusi yako.” Oya, watu walikuwa hawapoi, hawaboi. Ilikuwa kasheshe.

Lakini wakati watu wanashangilia harusi hiyo mimi nilikuwa natazama kwa huzuni jinsi tasnia ya muziki Bongo inavyozidi kujipambanua kwamba ilishaacha kuwa tasnia ya muziki kitambo na sasa imekuwa tasnia ya maisha ya wanamuziki. Nitakueleza kwanini.

Mara ya mwisho Jux alitoa albamu ya muziki 2023. Albamu ilikuwa inaitwa King of Hearts na ilikuwa na hits song za kutosha tu ikiwemo Lucky Now aliyomshirikisha Bien, I’ll be There aliyomshirikisha Patoranking, Nidhibiti aliyoimba na Zuchu… yaani ngoma kali zilikuwa kibao kwenye albamu hiyo. Lakini wakati anaiachia haikupata ‘atensheni’ hata robo aliyoipata kwenye harusi yake.

Na si yeye tu, Darassa ameachia albamu majuzi kati lakini haikufikia ukubwa wa atensheni ya harusi ya Jux. Marioo ameachia albamu hivi karibuni pia haikufikia ukubwa wa harusi ya Jux.

Kwa kifupi ni kwamba biashara ya muziki kwa sasa imehama kutoka kutengeneza muziki na kuwa kutengeneza stori kuhusu mwanamuziki.

Ni kama vile hakuna anayezingatia msanii ameachia ngoma. Bali watu wanataka kujua tu msanii ameachwa na demu gani? Kama unabisha, jaribu kuangalia trendi ya matukio ya mwisho kutrendi mitandaoni yalikuwa yanahusu nini… tukianza na harusi ya Jux kuna harusi ya Hamisa na Aziz Ki, kuna kuachana kwa Zaylisa na Manara, Zuchu na Lisa kumgombania Diamond, wasanii wa Bongo kudaiwa kuzingua Trace, Zuchu na Diamond kutibuana na stori zingine za aina hiyo.

Uzuri ni kwamba matukio yote ya aina hii yanawaingizia wasanii wetu pesa kwa namna moja au nyingine.

Lakini ukweli ambao tutajaribu kuukimbia kuna siku utatufukia na kututafuna ni kwamba tasnia inayoegemea kwenye matukio kuhusu wanamuziki kuliko muziki haina afya na inaua matumaini kwa wasanii wenye vipaji vya kufanya muziki kwa sababu watakuwa wanafanya na hakuna anayewazingatia.

Kwa sababu pesa haipo kwenye kuimba, ipo kwenye maisha ya muimbaji. Hapa ni aima tuangalie namna ya kubadilika au tusubiri siku ya sanaa kuzikwa mazima.