Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Snura Mushi : Naweza nisifike peponi

SNURA Pict

Muktasari:

  • Julai 2024 Snura alitangaza kuacha muziki rasmi,na  akaomba nyimbo zake zisipigwe tena. Snura Mushi alitangaza kuacha rasmi muziki na shughuli za kisanaa na kujikita zaidi kwenye dini.

Dar es Salaam. Licha  ya kwamba kwa sasa ameishika dini vilivyo, aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya hususani singeli na filamu, Snura Mushi amewaomba watu wamuombee ili aweze kufika peponi.

Akizungumza na Mwananchi, Snura alisema anaweza kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha watu waache dhambi na kuyafuata anayopenda Mungu, lakini asifike peponi kama watu wanavyotarajia.

SNURA Pict

“Unajua japo mimi natumia muda mwingi sana kwenye kurasa zangu za kijamii kuwahamasisha watu waache mabaya lakini wanaweza kuingia peponi wasinione hivyo nawaomba sana waniombee na mimi niweze kuuona ufalme wa Mungu nawaomba sana,” alisema Snura.

Julai 2024 Snura alitangaza kuacha muziki rasmi na  akaomba nyimbo zake zisipigwe tena. Snura Mushi alitangaza kuacha rasmi muziki na shughuli za kisanaa na kujikita zaidi kwenye dini.

Alizitaka media na watu binafsi kuacha mara moja kufanya hivyo kwa kuwa amebadilisha aina ya maisha yake kabisa.