Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Snura atangaza kuacha muziki, asema akifa ‘asipostiwe’ mitandaoni

Muktasari:

  • Mbali na hilo, msanii huyo amesema anajutia aliyokuwa akiyafanya kipindi akiwa kwenye sanaa.

Dar es Salaam, Mwanamuziki Snura Mushi ametangaza kuacha muziki huku akikataza nyimbo zake kuchezwa kwenye vyombo vya habari. Hatua hiyo imekuja baada msanii huyo kudai amemrudia Mungu.

"Watanzania na nje ya nchi mimi Snura leo natangaza rasmi kuwa nimeacha kazi za sanaa nilizokuwa nazifanya. Sababu kubwa ya kuacha ni kumrudia muumba wangu, nifuate dini yangu ya Kiislamu inavyosema na mwanamke wa Kiislamu anavyotakiwa kuwa," amesema Snura kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Mbali na hilo, msanii huyo amesema anajutia aliyokuwa akiyafanya kipindi akiwa kwenye sanaa.

"Nisiwe muongo najutia sana niliyoyafanya na maamuzi yangu ya kuacha sanaa niliyafanya miaka mingi iliyopita, mwanzoni wazo langu lilikuwa kuacha kimyakimya nisiseme kwa yeyote wala popote ijue tu familia yangu, ndugu zangu na watu wanaonizunguka lakini kwa sababu hivi vitu vinaishi miaka na miaka na vizazi vipya vinakuja sitaki kuwa sababu ya kuwaharibu," amesema.

Katika hatua hiyo ya kutangaza kuacha muziki pia ameomba nyimbo zake kuacha kuchezwa kwenye vyombo vya habari. 
"Nisingeweza kupita kila redio na Tv kuwakataza wasicheze nyimbo zangu, natumia fursa hii ndugu zangu kwa heshima na taadhima naomba sana mnipokelee ombi langu msicheze kazi zangu kabisa naomba mfute, fanyeni kama hakuna kilichotokea," amesema Snura.

Snura pia ameomba siku atakayofariki picha zake zisichapishwe kwenye mitandao ya kijamii.

"Ukisikia nimekufa umehuzunishwa na msiba wangu njoo unizike kama ni mwanamke usije mtupu njoo na stara, picha ambazo hazina heshima msiposti hayo mapicha wala madude dude kwa sababu naona tukifa hayo madude ndiyo mnaposti," amesema.

Baadhi ya ngoma alizowahi kutamba nazo Snura kabla ya kutangaza kuacha muziki ni ‘Majanga’, ‘Nimevurugwa’, ‘Chura’, ‘Shoga Yake Mama’, ‘Ushaharibu’ na ‘Shindu’.

Hii itakuwa si mara ya kwanza kwa msanii kutangaza kuachana na kazi za sanaa na kumrudia Mungu. Mwaka 2016 mkali wa miondoko ya muziki wa taarabu, Mzee Yusuph alitangaza  kuacha kazi za sanaa na kumtumikia Mungu. Hata hivyo mwaka 2020 alirudi tena kwenye kazi za sanaa alizokuwa akifanya awali.