Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la Said kwa Rais Samia lamfikia Leonardo

Muktasari:

  • Leonardo ameyasema hayo wakati akizungumza na Mwananchi, ikiwa kunaendelea vuguvugu kwenye mitandao ya kijamii, likidai utumbuizaji wa Said Said mbele ya Rais Samia haukuzingatia heshima na adabu

Dar es Salaam. Mchekeshaji Leonardo Butindi 'Leonardo' amesema haamini maneno ya watu yanayodai kuwa pafomansi ya Said Said mbele ya Rais Samia Suluhu itaenda kuwazibia milango wasanii wa vichekesho.

Leonardo ameyasema hayo wakati akizungumza na Mwananchi, ikiwa kunaendelea vuguvugu kwenye mitandao ya kijamii, likidai utumbuizaji wa Said Said mbele ya Rais Samia haukuzingatia heshima na adabu.

"Sidhani kama serikali yetu inaangalia makosa sana kiasi hicho. Ameteleza kidogo ni mtoto tupewe fursa nyingine tasnia bado inakuwa ni vizuri tujifunze.Unajua wanasema pafomansi isiendane na mihemko, wakati mwingine ikitokea jokes ikienda vizuri au ikiwa mbaya mambo yanayumba. Lakini yote ni katika kujifunza simlaumu.

"Yale mawe mimi huwa nayapokea nikizingua na yanauma lakini yanajenga. Hata shoo ya kwanza ya tuzo za comedy ambayo sikupiga vizuri sana nilipokea mawe ambayo yalifanya hii shoo nijipange vizuri zaidi, pengine na yeye atapokea ili yamjenge. Mawe ni muhimu hata Diamond anapigwa mawe,"amesema

Hata hivyo, kutokana na wao kufanya ucheshi unaoendana wote wakizungumzia ishi ya Kajala na Harmonize, Leonardo amesema kawaida katika ucheshi maudhui hayatakiwi kujirudia.

"Mimi sina uhakika kama nilimwambia nitaongelea Kajala na Harmonize. Lakini ikitokea mtu akapanda ikagusa kitu chako, unatakiwa kukipigia mstari kwamba hiki sikisemi tena. Unajua kazi zetu ukiona mambo hayaendi vizuri unaanza kutafuta pakutokea. Ilitakiwa ya Harmonize ikae pembeni ndiyo huwa tunafanya hivyo,"amesema.

Utakumbuka Leonardo alianza kupanda jukwaani na kufanya utani wa kumwambia Rais Samia kuwa Kajala na Harmonize wamerudiana hata hivyo, baadaye alipopanda Said naye alirudia ucheshi huohuo. Jambo lililopelekea wengi kudai aliishiwa ubunifu.

Leonardo amesema ni vyema msanii wa vichekesho kuzingatia muktadha aliyepo kabla ya kuzungumza jambo.

"Ucheshi uendane na mazingira, sehemu ya watu wengi heshima lazima iwepo maneno ambayo unatumia yaendane na sehemu husika. Kwa hiyo nimefanya yangu yameenda vizuri Said ndiyo hivyo anapata maneno ukikosea sehemu unajifunza tasnia ifike mbali," alisema Leonardo.

Utakumbuka hayo yote yalitokea jana Mei 5, 2025, katika usiku wa Samia Kalamu Awards, zilitolewa katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam. Huku Rais Samia akiwa ndiye mgeni rasmi.