Prime
Said awatolea uvivu wanaoponda alichokifanya kwa Samia

Muktasari:
- Said ambaye amezua mijadala kwenye mitandao ya kijami kutokana na pafomansi yake aliyoielekeza kwa Rais Samia, amejikuta akipokea maoni mbalimbali ya ukosoaji kwenye mitandao ya kijamii wengi wakidai haikuwa ya heshima.
Dar es Salaam. Mchekeshaji Said Said ameiambia Mwananchi kuwa alichokifanya jana Mei 5,2025 kwenye usiku wa tuzo za Samia Kalamu Awards, kiliwafurahisha waliomualika hivyo wanaomponda kwenye mitandao ya kijamii hawampi shida.
Said ambaye amezua mijadala kwenye mitandao ya kijami kutokana na pafomansi yake aliyoielekeza kwa Rais Samia, amejikuta akipokea maoni mbalimbali ya ukosoaji kwenye mitandao ya kijamii wengi wakidai haikuwa ya heshima.

"Hao wote wameandika walivyoona, mimi pafomansi niliyoenda kufanya pale nimealikwa na watu wa 'event' na serikali ilimradi wameinjoi na wamenipongeza mimi mengine sijui. Dokta Tulia Ackson (Spika wa Bunge), kanipongeza yaani viongozi wote wamenipongeza. Tulia kaniambia nipo sawa halafu mtu yupo Mpigi Magohe anasema mimi nimekosea nianze kumuwaza,"amesema Said.
Hata hivyo, mchekeshaji huyo hakuishia hapo amesema siyo vibaya kwa yeye kumpa taarifa Rais ya Kajala na Harmonize kurudiana, hata kama mchekeshaji mwenzie Leonardo alifanya hivyo awali.
"Kwani Leonardo ndiyo ana taarifa za Harmonize kurudiana na Kajala peke yake. Sasa wote tumemwambia mama kuna ubaya gani,"amesema Said.
Utakumbuka hayo yote yamejiri baada ya ukosoaji mkubwa wa pafomasi yake kwenye usiku huo wa tuzo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Mei 6,2025.

"Lazima ujue unaongea nini mbele ya nani. Rais tuliyenaye ni mama mwenye upendo sana, tusiharibu tukashindwa kufaidi matunda ya upendo wake kwetu. Jana nimeona Said anaongea vitu ambavyo watu hawacheki tena bali wanaogopa.
"Halafu akataka kuharibu zaidi kwa kwenda kumpa cheni Rais bila kuwa amewasiliana na walinzi wake. Siku nyingine ukitaka kumpa zawadi Rais waambie walinzi wake siku tatu kabla ili wajiandae kwa hilo tukio usijaribu ku-suprise Rais. Kinachokuponza mdogo wangu dharau na hauna adabu.
"Sasa utasababisha mkialikwa. Kwenye event kama hizo muanze kukaguliwa vichekesho vyenu kwanza kwa kuwachekesha walinzi 'back stage' ili waediti vichekesho vyenu na hiyo itawanyima uhuru kwa namna moja au nyingine,"ameandika Baba Levo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Naye Fredrick Bundala kupitia ukurasa wake wa Instagram alitoa ukosoaji wake kwa kuandika "Jana ucheshi wake haukuwa comfortable. Aliharibu, anakoelekea anaweza asipate tena fursa ya kupanda mbele ya mheshimiwa!
"Dakika za mwanzoni alianza vizuri hasa alipompa mrejesho wa ile picha ya mwanzo! Ila akanogewa na kuanza kutoka nje ya mstari hadi kurudia joke ya Leonardo kuhusu Konde na Kajala!,"

Haikuishia hapo naye Hajathe Credible kupitia ukurasa wake wa X alichapisha ujumbe usomekao "Huyu Said Said Sasa Ataharibu, Mimi Siridhishwi na Aina ya Ucheshi Wake Mbele ya Kiongozi Mkuu. Ile Kuonesha Anamuweza, Jokes za Kumfanya Ni kama mtu Wakawaida While Ni Amiri Jeshi Mkuu, Hii Hapana, I think Leonardo He’s doing great. Atawaharibia Wengine Sasa,"
Utakumbuka tuzo hizo za Samia Kalamu Awards, zilitolewa jana Jumatatu Mei 5, 2025 katika ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam. Huku Rais Samia akiwa ndiye mgeni rasmi.