Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu ya Jay Moe kufanya kazi nyingi na Ngwea 

Muktasari:

  • Huyu ni miongoni mwa wasanii waliounda kundi la Wateule ambalo lilisainiwa Bongo Records, lebo ambayo ilisimamia albamu mbili za Jay Moe ambazo zilimpa jina katika tasnia na kumtengenezea heshima aliyonayo sasa.

Dar es Salaam, Kwa miaka zaidi ya 20 katika muziki, Jay Moe amejizolea sifa kama rapa mwenye uwezo mkubwa wa kuandika mambo ya kufikirisha na kuchana katika mtindo unaovutia na kushawishi kusikiliza kwa muda mrefu.

Huyu ni miongoni mwa wasanii waliounda kundi la Wateule ambalo lilisainiwa Bongo Records, lebo ambayo ilisimamia albamu mbili za Jay Moe ambazo zilimpa jina katika tasnia na kumtengenezea heshima aliyonayo sasa. Fahamu zaidi.

Jay Moe alianza muziki na kundi la Wateule mwaka 1998 akiwa na wenzake kama Mchizi Mox, Solo Thang na Jaffarai, pia kuna Lady Lou na Mack 2B ambao tayari wametangulia mbele ya haki. Kabla ya kundi hilo kuundwa, Jay Moe, Mchizi Mox na Jaffarai walikuwa marafiki wenye kiu ya kufanya muziki ambao walikuwa wanaishi mtaa mmoja, Makumbusho, Dar es Salaam.

Wakiwa katika harakati za muziki, shule iliwatenganisha, Mchizi Mox na Jay Moe walienda kusoma Mbeya ila shule tofauti. Vivyo hivyo kwa Jaffarai naye akashika njia yake kimasomo ila kila likizo walikutana na kuendelea na muziki.

Baadaye Jay Moe, Mchizi Mox na Jaffarai wakaibuka washindi katika shindano la kusaka vipaji vya muziki ambapo P-Funk Majani na Master J walikuwa ndio majaji, na ndio ikawa njia ya wasanii hao kufahamika kwa ukubwa.

Mwaka 2000 kundi la Wateule walisainiwa na lebo ya Bongo Records chini ya P-Funk Majani na ukawa mwanzo wa kutoa nyimbo zao zilizofanya vizuri kama Msela, Si Ndio, Pengo, Nipende Au Nichukie, Tumerudi Tena, Vile Vile na kadhalika

Hata hiyo, Solo Thang kutoka Wateule na Juma Nature ndio wasanii wa kwanza kusainiwa Bongo Records katika mtindo wa kibiashara, ila awali lebo hiyo ilishafanya kazi na Dolla Sol, Hashim Dogo na kundi la No Name ambalo Majani pia alikuwepo.

Mwaka 2001 ndipo Jay Moe akasainiwa Bongo Records kama solo na kufanikiwa kutoa albamu zake mbili, Ulimwengu Ndio Mama (2002) na Mawazo ya Jay Moe (2004) ambazo zilifanya vizuri wakati huo. Albamu yake, Ulimwengu Ndio Mama (2002) ilikuja baada ya Jay Moe kujifunza vitu vingi kwa kuwatazama walimwengu kwani mama’ke mzazi alifariki akiwa mdogo, hivyo hakupata nafasi ya kufunzwa naye kwa muda mrefu.

Jay Moe aliandika wimbo wake, Maisha ya Boarding (2002) baada ya kwenda kusoma shule ya kulala huko Mbeya, kutokana na kukulia maisha ya kishua aliona maisha mapya ya shule ni magumu sana ila baadaye akagundua ni sehemu ya kujifunza.

Baada ya Ngwea kufanya vizuri na wimbo wake, Ghetto Langu (2002) aliourekodi kwa Sh100,000, Jay Moe alimshawishi sana Majani kumsaini rapa huyo Bongo Records. Majani alikubali na ndipo Ngwea akaja na albamu yake iliyofunika sana, A.K. A Mimi (2004).

Kundi la Wateule lilikuwa na ukaribu mkubwa na lile na Chemba Squad liloanza mwaka 1999 likiwa na wasanii kama Ngwea, Mez B, Dark Master na Noorah, na ndio sababu Jay Moe na Ngwea waliweza kufanya kazi nyingi pamoja. Baadhi ya nyimbo ambazo Jay Moe na Ngwea wameshirikiana ni Mikasi, Mida Mibovu, Kimya Kimya, Cheza Kwa Step, Unisamehe na kadhalika. 

Wimbo wa TID na Jay Moe, Girlfriend (2002) uliotumika kama soundtruck ya filamu ‘Girlfriend’ ulirekodiwa wakati Jay Moe, AY,  King Crazy GK, Nina na Monalisa wa’shamaliza kushuti filamu hiyo ambayo ilipata mapokezi mazuri.

Na filamu hiyo ilimpatia Jay Moe fedha nyingi  kwa sababu alilipwa kama mwigizaji, akalipwa fedha ya soundtruck na pia kama mtumbuizaji katika hafla za uzinduzi ambapo alifanya shoo mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Mwanza.