Ray C awapa funzo wasanii Bongo

Muktasari:
- Kauli hiyo ya Ray C imekuja baada ya wasanii wa kike kutoka nchini Nigeria Tems na Ayra starr kuonekana kwenye video wakiimba na kufurahi pamoja, wimbo uitwao Commas, wa Ayra Starr uliotoka miezi miwili iliyopita.
Mwanamuziki Rehema Chalamila, maarufu kama Ray C ametoa fuzo kwa wasanii nchini Tanzania, kudumisha upendo ili kazi zao ziweze kufanya vizuri zaidi.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ray C ameandika kuwa wasanii wapendane wenyewe kwa wenyewe kwani mioyo yao ikiwa safi lazima milango itafunguka zaidi.

"Halafu mnajiuliza mbona kama game ya TZ imestuck? Pendaneni wenyewe kwa wenyewe kwanza, mioyo yenu ikiwa safi ndani mkapendana wenyewe kwa wenyewe kwanza lazima milango mikubwa zaidi itafunguka kama inavyozidi kuwafungukia hawa wenzetu. Siyo mambo ya kuchekeana usoni mkipeana migongo mnang'ong'ana". Ameandika
Kauli hiyo ya Ray C imekuja baada ya wasanii wa kike kutoka nchini Nigeria Tems na Ayra starr kuonekana kwenye video wakiimba na kufurahi pamoja, wimbo uitwao Commas, wa Ayra Starr uliotoka miezi miwili iliyopita.
Utakumbuka Ray C alitamba miaka ya 2000 na ngoma zake kama vile Wanifuata nini, Mapenzi Yangu, Sogea Sogea, Uko Wapi, na nyingine nyingi.