Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyuma ya pazia Jennifer Lopez na Ben Affleck kuuza jumba lao

Muktasari:

  • Wakati uvumi ukiendelea kushika kasi kuwa Jennifer Lopez (J.Lo) ameachana na mumewe Ben Affleck, inaripotiwa kuwa wawili hao wanauza jumba lao la kifahari la Beverly Hills ambalo walilinunua kwa Dola61.8 milioni

Marekani, Wakati uvumi ukiendelea kushika kasi kuwa Jennifer Lopez (J.Lo) ameachana na mumewe Ben Affleck, inaripotiwa kuwa wawili hao wanauza jumba lao la kifahari la Beverly Hills ambalo walilinunua kwa Dola61.8 milioni.

Affleck, 51, na Lopez, 54, ambao wamecheza pamoja filamu, Gigli (2003) na Jersey Girl (2004), wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo tangu Juni 2023 walipopigwa picha huko Los Angeles, Marekani  wakiwa ndani ya duka kubwa wakichagua samani.

"Affleck hakuwahi kuipenda nyumba hiyo. Iko mbali sana na watoto wake." Kinasema chanzo cha karibu. Kuhusu Lopez, chanzo  hicho kilieleza kuwa nyumba hiyo ni kubwa sana kwake kwa sasa.

Kulingana na Wall Street Journal, jumba hilo lenye ukubwa wa futi za mraba 38,000 ndani ya eneo la ekari 15, lina ukumbi wa sinema, bwawa la kuogelea, saluni, viwanja vya michezo, vyumba 12 vya kulala, bafu 24, majiko 15 na eneo la kuogesha magari 15.

People wanaripoti kwamba tangu mwezi Mei Affleck amekuwa akiishi katika nyumba ya kupanga maili chache kutoka kwenye jumba la kifahari huku akitengeneza filamu yake ya The Accountant 2, wakati huo Lopez akiishi pekee yake katika nyumba hiyo.

Wawili hao ambao mwaka 2003 waliairisha harusi yao kutokana na kuandamwa na vyombo vya habari, walionekana pamoja mara ya mwisho walipohudhuria mchezo wa mpira wa vikapu pamoja na mtoto wa Affleck, Samuel, 12, huko Santa Monica, California Juni 2.

Habari za kuuza nyumba yao zinakuja zaidi ya wiki moja baada ya Lopez kutangaza kuairisha ziara yake ya muziki, This Is Me... Live kwa kile kilichoelezwa kuwa anachukua muda wa kupumzika ili kuwa karibu na watoto wake, familia na marafiki wa karibu.

Utakumbuka Lopez na Affleck walikuwa na uhusiano mwaka 2002 hadi 2004 walipoachana, Lopez akaenda kufunga ndoa na Marc Anthony (2004 - 2014) na kujaliwa watoto wawili, huku Affleck akimuoa Jennifer Garner (2005 - 2018) na walijaliwa watoto watatu.

Hata hivyo, walikuja kurudiana Julai 2021 ikiwa ni 17 ya utengano, walichumbiana kwa mara ya pili Aprili 8, 2022 na walifunga ndoa huko Las Vegas hapo Julai 16, 2022 ikiwa ni ndoa ya nne kwa Lopez baada ya kuoana na Ojani Noa (1997), Cris Judd (2001) na Marc Anthony (2004).