Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya boksi: Khadija Kopa na Jide hadi Nandy na Zuchu

Muktasari:

  • Anaimba wimbo wa Tx Mpenzi. Mbele ya halaiki ya watu. Wakiimba naye kila mstari. Manjonjo meengi yenye huba ndani yake. Kiswahili cha Paje, lafudhi ya Bububu. Ligha adhimu ya kiswahili na nakshi nakshi za matanshi.

Dar es Salaam. Kwa wahenga. Vuta kumbukumbu ya mwanadada mweusi. Weusi ule wenye kung’aa kama mchaichai. Ngozi yake nyororo, mwili flani wenye afya njema. Mcheshi kweli kweli, meno na macho meupe peee.

Anaimba wimbo wa Tx Mpenzi. Mbele ya halaiki ya watu. Wakiimba naye kila mstari. Manjonjo meengi yenye huba ndani yake. Kiswahili cha Paje, lafudhi ya Bububu. Ligha adhimu ya kiswahili na nakshi nakshi za matanshi.

Muite Bi Khadija Kopa. Tuliomuona na kumsikiliza enzi hizo kabla ya Y2K? Ni raha kukumbuka kumbukizi zake. Yes, alikuwa mwanadada fulani wa nyakati usimguse. Mtoto wa mjini kweli. 

Hii ngoma ya Tx Mpenzi usipime hata nusu. Bonge la ngoma. Ni hit song la kweli bila kutegemea drama na kiki. Ni kila nyumba wimbo linaunguruma kwa vinanda. Kwa gitaa la besi na vingoma flan amazing. 

Staa kweli kweli Khadija Kopa. Kutoka Mwananyamala mpaka Kurasini Shimo la Udongo. Toka Mabibo Jeshini hadi Mlalakuwa kwa Alfred Kimaro. Dada huyu alikuwa na jina kubwa na ngoma zake zilikuwa maarufu. 

Sijui. Lakini kumbukumbu zangu hilo pini lilipiga pini. Serikali ya Komando Salmini Amour, nadhani walipiga stop wimbo huo usichezwe. Kuanzia radio mpaka shughuli za kuwatoa mwali. Ni pini flani.

Kama adhabu yake imeisha ni vyema mtu akalirudia. Walah wabilah mwezi Mtukufu huu wa Ramadhan. Nasema kwamba, atakayeirudia hili dude nina uhakika atasomba kijiji kizima na miti yake. Tx Mpenzi? Nomaa.

Ule ni wimbo ambao ulitolewa kabla ya wakati. Ulipaswa kutolewa mwaka 2040. Wakati huo Rais wa Tanzania amezaliwa mwaka 2000. Ila Khadija alitoa hili pini wakati Nyerere ana wiki moja toka atoke Ikulu.

Miaka ya 2000 akaibuka mwandada mwingine. Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide, Wallet, Mama Some Food, Komando. Kama Bi Khadija na Jide naye akawa staa mkubwa wa kike. Noma na nusu.

Tofauti ni kwamba Kopa ni taarabu na Jide ni Bongo Fleva (R&B). Jide naye katika zama zake alikuwa ni nembo ya nchi. Kuanzia Kiwalani mpaka Kona ya Bwiru. Kutoka Nzovwe mpaka Njiro. Ni Jide tu.

Bongo Fleva ikiwa inachanua kushika kasi yake. Mabishoo wakichana pini za Hip hop. Sista Duu Jide alikuwa na dunia yake ya kupamba korasi za hao masela na mabishoo. Jide kapamba sana ngoma za wana.

Jide alikuwa ‘akidisi’ wewe ‘unashaini’, akikusifu ‘unashaini’. Yaani kinywa chake kilipotumika vyovyote kukaja jina tu. Ungepelekwa maduniani. Hebu fikiria kama mashairi tu, kila mtu kwa wakati walitafsiri ajuavyo.

Ubora wa Jide haukuwa kwenye sauti tu. Bali kwenye utunzi bora na zaidi ni kujua nini anafanya na kwa ajili gani. Ni kwamba ni mmoja wa wanamuziki wachache sana wanaojitambua na pia kujikubali.

Asingejikubali Jide, angepotea. Na pia asingejitambua angebaki historia tu. Binti Komando kweli, misimamo na ile hasira ya maisha, ikamsafirisha toka kwenye muziki wa CD tu mpaka kuwa na bendi. Machozi Band. 

Naweza kusema yeye ndo aliyefungua akili za wengi kuanzisha band. Wengi wao wamekuja baada ya bendi yake nao wakaleta zao. Na kwenye shoo za bendi nako alikaza kinoma kiasi cha kuwatisha hata Twanga na wenzao.

Unakumbuka Ghounzhou, pale mbele ya Victoria? Watoto wa mjini woote ungewakuta pale. Kila wikiendi wana tungefika pale. Siyo kumsapoti bali kuburudika na muziki na kutazama pisi za maana. 

Kuna mabwege wana tabia ya kusema tunaenda kumsapoti. Nenda kasapoti dada zako. Ukweli wengine hatukufika pale kusapoti, bali kuburudika na Jide. Unamsapoti vipi anayekupa furaha? 

Vita ikawa kubwa. Akatolewa pale akahamia Thai Village. Nako akawa na nyomi kuliko Ghounzhou, nako akafanyiwa figusi. Akaona isiwe tabu, akaanzisha Nyumbani Lounge ya kwake. Kwisha habari.

Na sasa kuna Nandy na mtoto Zuchu. Hawa ni wa nyakati hizi za Instagram na WhatsApp. Hawa wanafuata kwa dada na mama yao. Namuona Nandy katika mwili wa Lady Jaydee. Huyu ni Jide wa sasa.

Na namuona Zuchu kwenye mwili wa mama yake Khadija Kopa. Kuna vitu vya Nandy anavyo Zuchu hana ama hajatuonesha. Na kuna vitu vya Zuchu ambavyo Nandy hana au hajaonesha. Ndiyo. 

Zuchu anaandika sana, na uandikaji wake siyo poa. Na Nandy anajua sana kujisimamia. Na sidhani kama kuna msanii wa kiume miaka ya karibuni mwenye uwezo huu. Haya ni majembe ya kike nchini kwa sasa.