Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miradi 10 ya ubunifu yalamba ruzuku ya Sh 270 milioni

Muktasari:

  • Ruzuku hizo zimewekwa kwa ajili ya kusaidia miradi ya sanaa na utamaduni zinazohusiana moja kwa moja na jamii ya Kitanzania. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space, Lilian Mushi, ameelezea umuhimu wa ruzuku hizo katika ukuaji wa sekta ya sanaa nchini.

Dar es Salaam. Katika hatua ya kukuza ubunifu na sanaa nchini Tanzania, wabunifu kumi wamepokea jumla ya Sh270 milioni kupitia 'Feel Free Grant 2025', mpango unaoratibiwa na 'Nafasi Art Space' kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa. Mpango wenye lengo la kuhamasisha uhuru wa kisanii, uvumbuzi na kuwaleta wasanii karibu zaidi na jamii wanazozihudumia.

Ruzuku hizo zimewekwa kwa ajili ya kusaidia miradi ya sanaa na utamaduni zinazohusiana moja kwa moja na jamii ya Kitanzania. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space, Lilian Mushi, ameelezea umuhimu wa ruzuku hizo katika ukuaji wa sekta ya sanaa nchini.

“Mpango wa Feel Free ni daraja muhimu kati ya wasanii na msaada wanaohitaji kutekeleza miradi yao. Tumeweza kuchagua miradi kumi bora baada ya mchakato wenye ushindani mkubwa. Kwa mwaka huu 2025, kila mmoja wa washiriki waliochaguliwa amepokea kati ya Sh 17 milioni hadi Sh25 milioni. Miradi hii itatekelezwa katika maeneo mbalimbali kama Mtwara, Dar es Salaam, Zanzibar, na maeneo mengine nchini,"amesema Lilian.

Mbali na Lilian mwenyekiti wa bodi 'Nafasi ART' Risha Chande amesema mchango wa sanaa katika maendeleo ya jamnii ni muhimu.

"Sanaa inagusa sehemu tofauti ya ubongo wetu kama hisia zetu, pamoja na kusema inatusaidia kubadilisha fikra, pia ni chanzo cha kipato kwa vijana. Sisi tumehakikisha wasanii wa kila kona wanatambulika na wanaweza wakapata fursa za kujiendeleza, kuonesha sanaa zao kwa watu wengine,"amesema 

Miongoni mwa miradi iliyonufaika ni ule wa  Scolastica Mwambete, ambaye analenga kufufua hamasa ya vijana katika sanaa ya uchongaji. Akiamini kuwa sanaa hiyo inapuuzwa.

Scolastica amepanga kuendesha mafunzo ya miezi mitano kwa vijana mkoani Mtwara, ili kuwapa mbinu mpya za kisanaa na uwezo wa kutumia sanaa kama chombo cha kujieleza na kujenga mijadala ya kijamii.

“Uchongaji una uwezo mkubwa wa kuibua mijadala kuhusu masuala ya sasa. Tunataka vijana waone thamani ya sanaa hii na kuitumia kama njia ya kushiriki katika mabadiliko ya kijamii,” amesema.