Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Millen Magese jaji mkuu Samia Fashion Festival

Muktasari:

  • Mwanamitindo huyo ambaye anaishi nchini Marekani kwa sasa, alisema uandaaji wa Vazi la Samia ni alama ya stara, uongozi na heshima, hivyo ni zaidi ya mavazi ya kawaida na kubeba kazi ya sanaa inayostahili kuhifadhiwa katika makumbusho kwa vizazi vijavyo.

Dar es Salaam. Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Magese ametangazwa kuwa Jaji Mkuu wa Tamasha la Samia Fashion Festival litakalofanyika Novemba 30 mwaka huu visiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi leo Novemba 28, 2024, Millen Magese amesema hiyo kwake ni heshima kubwa na ana furaha kusimama kama Jaji Mkuu wa Samia Fashion Festival na kwamba anajivunia kushuhudia wakati huu wa kihistoria ambao unasherehekea ubunifu, stara na urithi wa kipekee wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Kwa zaidi ya miaka ishirini, nimejitolea maisha yangu katika sekta ya mitindo na urembo, nimezunguka duniani, nikifanya kazi na chapa kubwa na maarufu, nimeona jinsi mitindo inavyothaminiwa katika nchi za Ulaya na mataifa mengine, si tu kama sanaa bali kama alama ya utambulisho, urithi na fahari.
 
“Niliposikia kuhusu mpango huu wa kipekee, sikusita, nilichukua ndege haraka kuja nyumbani kuwa sehemu ya safari hii ya kihistoria, kwa tamasha hili si tu kuhusu mavazi; ni kuhusu heshima yetu kama Watanzania,” alisema.

Mwanamitindo huyo ambaye anaishi nchini Marekani kwa sasa, alisema uandaaji wa Vazi la Samia ni alama ya stara, uongozi na heshima, hivyo ni zaidi ya mavazi ya kawaida na kubeba kazi ya sanaa inayostahili kuhifadhiwa katika makumbusho kwa vizazi vijavyo.

Mbali na Magese kuwa jaji mkuu, wengine ni Idris Sultan, Khadija Mwanamboka, Jokate Mwegelo, Martin Kadinda, Faraja Nyalandu na Nancy Sumari.

Awali akizungumza kuhusu Samia Fashion Festival, Mwanzilishi na Muandaaji wa Tamasha hilo, Khadija Mwanamboka alisema amewashirikisha wanamitindo mbalimbali na kuungana nao ili kusaidia watoto wanaoishi na virusi Vya UKIMWI na Saratani.