Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama afichua siri nzito ya Aziz Ki, Hamisa

Muktasari:

  • Stephane Aziz Ki amemtolea mahari ya ng’ombe 30 mchumba wake Hamisa ambaye anatarajia kumuoa siku za hivi karibuni.

Dar es Salaam. Mama mzazi wa Hamisa Mobetto aitwae Shufaa Lutenga maarufu 'Mama Mobetto 'amefichua siri akieleza siku ya kwanza mkwewe, Stephane Aziz Ki kukutana na Hamisa alimtamkia kuwa anataka kumuoa.

Mama Mobetto amesema hayo leo Februari 15, 2025 alipohudhuria tukio la mwanaye kuvalishwa pete katika viwanja vya Gofu Lugalo, Dar es Salaam.

"Mimi na Hamisa jinsi tunavyoishi huwa hatufichani kitu, na siku ya kwanza Hamisa kukutana na Azizi Ki alikuja kuniambia kuwa alimtamkia anataka kumuoa, sikuamini," amesema mama Mobetto.

Mama huyo, amesema, Hamisa na Azizi Ki wapo katika uhusiano mwaka moja hadi kufikia hatua ya sasa ya kufunga ndoa.

Amesema, anamshukuru Mungu Kwa tukio hili, kwani kuna mambo mengine mabaya yameongelewa kwake, ila Mungu ndio mtu wa mwisho mwenye kuamua kila kitu.

"Yamepita mambo mengine sana mazuri, na mabaya mengine sana, ila nashukuru Mungu kwa kila kitu, Hamisa ni mtoto wangu wa pekee nilikuwa naumia sana na maneno ya watu huko mitandaoni na wengine nje ya mitandao. Sasa ni wakati wa furaka kwake mwanangu."

Mama Mobetto amesema pia, Aziz Ki ndiye aliyemvalisha siku ya leo ya kupokea mahari.

"Kiukweli nimepata mkwe mwenye upendo sana, hizi nguo za leo nilizovaa ameniletea yeye, gauni hili ni Sh5 milioni na pochi Sh4 milioni," amesema.