Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maisha ya Hamisa Mobetto katika dunia ya Aziz Ki

AZIZ KI Pict

Muktasari:

  • Hamisa ambaye ni mke wa nyota wa zamani wa Yanga na kwa sasa anakipiga Wydad AC, Stephanie Aziz Ki amepitia changamoto nyingi miaka ya nyuma na kuandamwa sana mitandaoni, lakini hakukata tamaa na aliamini anachokifanya hadi sasa amejipata.

Dar es Salaam. Mwaka wake huu. Ndiyo, msanii mrembo na mjasiriamali, Hamisa Mobetto ana kila sababu ya kujiita mwanamke wa mwaka 2025, kwani yametokea mengi kwake na mengi ni mazuri.

Hamisa ambaye ni mke wa nyota wa zamani wa Yanga na kwa sasa anakipiga Wydad AC, Stephanie Aziz Ki amepitia changamoto nyingi miaka ya nyuma na kuandamwa sana mitandaoni, lakini hakukata tamaa na aliamini anachokifanya hadi sasa amejipata.

Ingawa mwaka 2025 haujaisha, lakini ni wazi kwa Hamisa ambaye alianza kujulikana akiwa kama mrembo wa video ‘video vixen’, kabla ya kuibukia uigizaji na uimbaji na sasa mjasiriamali, ndoa yake na Aziz Ki inazidi kuimarika.

Hapa Mwananchi linakuchambulia yaliyotokea kabla na baada ya ndoa hiyo ambayo inazidi kupumua tofauti na za mastaa wengi na zimekuwa hazidumu kutokana na misukosuko inayotokana na umaarufu wao na inaweza ikawa funzo kwao.

AZIZ 01

NI MWAKA WA HAMISA

Agosti 24, 2024, zilianza tetesi za uhusiano wa kimapenzi kati yao. Ni baada ya wawili hao kuonekana katika tamasha la Kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’ na Hamisa alivalishwa jezi ya Mwananchi na Aziz KI aliyeitwa jukwaani na mshereheshaji Haji Manara, kitendo kilichoibua shangwe kwa mashabiki.

Awali wawili hao walikuwa wanakanusha, kabla ya kuonekana tena wakishiriki picha za pamoja wakifurahia mapumziko ya kifahari (vacation) Dubai. Tukio hilo lilifuatiwa na mfululizo wa matukio ya ndoa yao na kisha harusi Februari 16.


AWAZIBA MDOMO WALIOMSEMA

Kabla ya ndoa mara kwa mara alikuwa akizungumziwa vibaya akihusishwa na wanaume matajiri na maarufu. Hata hivyo, mwenyewe hajawahi kulalamika kutokana na madai hayo na alipotezea.

Hata baada ya kuanza tetesi za ndoa, wengi waliona ni kiki kwa sababu ni msanii na labda anataka kuachia video akiwa na Aziz Ki, kabla ya tetesi hizo kuzimwa kwa kufanya kweli na kuvunja rekodi ya ndoa iliyofuatiuliwa na wengi ndani na nje ya nchi.

AZIZ 02

SIMU HAZIITI

Kwa mujibu wa Hamisa analiambia Mwananchi kuna mambo mengi yamebadilika baada ya kuwepo kwenye ndoa, ikiwamo kutokupata usumbufu kwa wanaomvizia na hiyo imempa heshima na uhuru wa kufanya kazi zake.


UMBALI WALA SIYO SHIDA YAO

Mwezi Mei, 2025, kulizuka maneno maneno mitandaoni ya kusema ndoa yao itavunjika muda siyo mrefu kutoka na Aziz KI kuondoka Tanzania.

Hata hivyo, Hamisa alizungumza na Mwananchi na kusema haachwi mtu na umbali kwao siyo tatizo, kwani atakuwa anaenda kwa mumewe kila wakati, hivyo anajua wazi watu wengi wanamhesabia siku kama ilivyo kwa mastaa wengine, lakini atawashangaza walimwengu wenye kusubiri ndoa za watu kuvunjika.

“Najua wazi watu watakuwa wananihesabia siku ndani ya ndoa yangu, lakini ukweli nitawashangaza watu wengi sana na sina sababu ya kuacha kuwa mke bora na mwenye heshima kwa mume wangu watanihesabia hadi watachoka wenyewe maana mimi nakomaa, nitakuwa naenda kwa mume wangu Kila wakati umbali sio tatizo kwangu,” alisema haya Hamisa Mobetto Kipindi cha Aziz KI kuondoka Tanzania.

AZIZ 03

KUTOKA KUJITAFUTA, KAJIPATA

Baada ya kujitafuta sana kuanzia ushiriki kwenye urembo ikiwamo kutwaa taji la Miss XXL, After School Bash 2010, aliendelea akishiriki mashindano mbalimbali yakiwamo mwaka 2011 mshindi wa pili Miss Dar Indian Ocean, mshindi wa pili Miss Kinondoni na kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania 2011 na 2012 alishiriki Miss University Africa na kuingia kwenye orodha ya warembo 10 bora.

Baada ya mashindano ya mrembo, aliamua kuanza kuchanga karata zake vizuri upande wa mitindo, uigizaji na muziki na kuzidi kujijengea jina na amewania na kushinda baadhi ya tuzo zikiwamo za Starqt Awards (2017) za Afrika kusini kipengele cha People Choice Awards, pia aliwania kipengele cha Super Mum ambacho  hakushinda.

Pia kashinda tuzo mbalimbali kutoka za kimataifa za Uganda, Nigeria.

Hamisa ni mmiliki wa Mobetto Styles, duka alililofungua tangu mwaka 2017.

Amepata dili nyingi za ubalozi wa kampuni mbalimbali mwaka huu na kuonyesha ndoa yake hiyo imekuja na kheri kwa kumfungulia zaidi milango ya riziki, kwani ni amesaini na kampuni zaidi ya 10 na anamiliki pia taasisi ya Mobetto Foundation Focus on education & health, pia Hatua na mobetto Mentorship kwa ajili ya wajasiriamali.

AZIZ 04

HESHIMA MTANDAONI

Kwa sasa heshima ya Hamisa imerejea mitandaoni na hakuna habari mbaya kumhusu huku wengi wakimsifia na kumpongeza kutokana na maisha yake kubadilika baada ya ndoa.


DENI KWA AZIZ KI

Amebakia na deni la ndoa yao kwa Aziz Ki, ambalo ni la kumpatia mtoto ili wazidi kujenga familia na hii itachangia pakubwa kuwanyamazisha wanaofuatilia maisha yao na kutaka kujua kama watadumu au la.


FUNZO KWA MASTAA

Tumeona ndoa nyingi za mastaa hazidumu, lakini ya Hamisa ni kama bahati haitetereki kwani hadi sasa amefikisha siku 335 sawa na miezi 11 tangu afunge ndoa na kabla alitabiriwa hafikishi hata miezi mitatu itavunjika.