Prime
Ndani ya Boksi: Hapa Hamisa kawaacha mbali Masista Duu Bongo
Muktasari:
- Mjengoni Dodoma. Mzee wa Kasi na Viwango Hayati Samuel Sitta kakalia kiti cha Uspika. Paula anaitwa Pau na Marioo hana a.k.a zaidi ya jina halisi la Omary Mwanga. Maximo akiwa bosi wa Stars na Ruge hamjui Mondi.
Dar es Salaam. Miaka hiyo. Staa mkubwa wa filamu akiwa Steve Kanumba na Ray Kigosi. Nyakati ambazo Mrisho Ngassa na Juma Kaseja wapo juu sana. Nyayo za Jakaya zikizitawala sakafu za Ikulu ya Magogoni. Maisha matamu.
Mjengoni Dodoma. Mzee wa Kasi na Viwango Hayati Samuel Sitta kakalia kiti cha Uspika. Paula anaitwa Pau na Marioo hana a.k.a zaidi ya jina halisi la Omary Mwanga. Maximo akiwa bosi wa Stars na Ruge hamjui Mondi.
Nipo mitaa ya Namanga. Chimbo flan hivi wanauza misosi na juisi. Kando yake kuna duka la vipodozi, ni pisi kali tupu zikiingia na kutoka. Hujui yupi wa Masaki yupi wa Tandika Maguruwe. Ni kwere jombaa mpaka nadata kabisa.
Kuna mtoto flan maji ya kunde mrefu hivi. Sura ya kimdolidoli. Akitabasamu ndani yake kuna Rihanna na Pricila wa Jux. Anakatiza mbele. Sioni umuhimu tena wa kula. Ninachokula nagundua ni feki, nikionacho ndo chakula safi.
Bado mbichi. Ngozi bado imenatana na mifupa kweli kweli. Tumbo lake ni gumu bado halijabebeshwa kiumbe. Sina ujasiri wa kuinuka kumfuata wala kumsemesha. Kwa sababu pembeni yangu nilikuwa na pisi nyingine. Noma.
Pisi niliyonayo ya moto kinoma. Lakini vidume tuna upimbi wa tamaa. Bado niliona nuksi kutopata mawasiliano ya yule mtoto. Niliendelea kula huku vita ikiendelea moyoni. Kinachouma ujue ni kwamba, Dar ukiiona pisi leo huioni tena.
Pembeni kulikuwa na wadada kadhaa wanakula. Wakaanza kuiongelea pisi ileile. Ikabidi nitege sikio vizuri kujua ni nani kupitia maongezi yao. Kumbe anaitwa Hamisa Mobetto, ni mshiriki wa mitindo na ulimbwende.
Baadaye nikaanza kumuona kwenye majarida mbalimbali. Mitandao na majukwaa ya urembo na shughuli nyingi za burudani. Akaendelea kuwa mrembo, mrembo zaidi ya jana. Mkato wa maana. Na baadaye amegeuka ni staa mkubwa.
Pesa haitafutwi. Ndiyo! Kwa sababu haijapotea. Pesa inategwa kwa akili na mipango. Ukichanganya na utulivu wa akili yako lazima utoboe. Hamisa Mobetto anatoa darasa kubwa sana kwa dada zetu. Ambao wengi wao ni vilaza.
Hamisa ameanza kupaa kiumaarufu katika mazingira tata. Lakini utulivu wa akili yake ulimsaidia kuwa pale alipo sasa. Utake usitake, kwenye hili la utulivu wa akili Missa anawaacha mbali sana mademu wa mjini. Mbalii.
Kuna mazingiria alipitia hapo katikati. Kwa akili mcharuko angedata kabisa. Utulivu wa akili yake ulimpeleka hadi kwenye muziki. Hasira za ‘eksi’ zake akataka kugeuza pesa. Kama Mondi na ‘eksi’ zake alivyowatumia kwenye gemu.
Misa ‘hakujimiksi’ na ‘grupsi’ kibwege. Alisimama kivyake na akifanya mishe zake kimya kimya. Misukosuko yake ya mapenzi na ‘eksi’ zake ilizidi kumpa jina. Huku akifanya vitu kwa hesabu na utulivu mkubwa. Noma sana!
Namba zikaongezeka kiutani utani tu kule Insta. Akawa mkubwa katikati ya pisi nyingi za mjini. Akaendelea kuwa mtulivu kwa kila hatua aliyopiga. Yes! Sapoti ya watu wengi aliipata na yeye alikuwa mnyenyekevu kwao. Ni silaha kubwa.
Kuna pisi zikipigwa chini zinawehuka. Zinataka kulipiza kisasi kwa kutoka na huyu mara yule. Kwenye hili utulivu wa Misa ndipo utauona. Alijiachia kidogo sana na Rick Rose na yule Mnaijeria sijui. Na hao alilazimika kufanya hivyo kwa sababu za kibiashara.
Lakini ‘majentromeni feki’ wa Kibongo hakutaka kujichoresha nayo. Utulivu wa akili yake umefanya awe juu hata leo. Huwezi kuona picha za ajabu za Missa. Huwezi kuleta video za kijinga za Missa. Wala huwezi kuleta sauti ya matusi ya Missa.
Mtoto ‘alikontroo’ gemu lake kikubwa sana. Anabaki kuwa mmoja kati ya pisi kali zenye majina na heshima kubwa mjini. Hili la utu na utulivu! Yes, limemfanya Misa awe dhahabu juu ya ardhi. Na kumfanya awe ndoto ya kila kidume mwenye akili zake.
Hata kwenye mitandao ya kijamii. Ni vigumu sana kukuta Missa anapewa maneno ya ajabu. Kuna mtindo bora wa maisha yake bila kuwa na macho ya rohoni kama mimi, huwezi kujua. Ni kwamba Missa ana dunia yake. Yes!
Nikikuuliza nitajie kampani ya Misa hapa mjini. Utakesha bila jibu. Pia nikikuuliza nitajie shost mkubwa wa Misa hapa mjini. Utakesha bila jibu. Kuna maisha aliyachagua Missa ndiyo yanayompa heshima mpaka leo. Na pesa pia.
Hii akili haipo kwenye vichwa vya pisi nyingi za mjini. Ni akili yenye kuhitaji kichwa chenye utu na utulivu kwanza. Na wenye utu na utulivu huu huishia kuitwa wachawi. Kwanza hupata vidume wenye pesa tu kwenye maisha yao.
Hakuna mwanaume anayetaka demu mapepe kama wa Kingwendu. ‘Neva’. Leo hii ukiacha ndoa yake na Aziz Ki, pia ana ndoa na kampuni nyingi za kibiashara. Hakuna kampuni ya kutoa dili kwa mtu mwehu mwehu. Utu na utulivu tu.
Utu na utulivu wa Missa ni mtego wa pesa. Aziz siyo mwehu kusaini kataba la pesa nyingi mbele ya Misa. Anajua yupo na mtu sahihi mwenye kichwa tulivu na chenye utu. Hajaoa karai au papai lile. Akili kubwa imeolewa pale.
Usimtazame Misa kwa mavazi yake. Usimtazame Misa kwa kitu kingine. Mtazame Misa kama safari tamu ya mtu mwenye utu na utulivu. Hatua zote za Misa ni elimu kwa dadaz wa mjini. Misa kawaacha mbali sana.