Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kopwe hashikiki Miss World, atinga kumi bora

Muktasari:

  • Halima ametinga katika hatua hiyo kufuatiwa na kampeni yake ya ‘Damu yangu, Kizazi Changu’ mradi ambao umelenga kuboresha afya kwa wanawake wajawazito na watoto nchini Tanzania ambao utasaidia kupunguza vifo kwa mama na mtoto.

Miss Tanzania 2022 ambaye anaiwakilisha nchi katika mashindano ya urembo duniani Halima Kopwe ametinga kumi bora katika kipengele cha ‘Beauty with Purpose Project’ kwenye shindano hilo linaloendelea nchini India.

Halima ametinga katika hatua hiyo kufuatiwa na kampeni yake ya ‘Damu yangu, Kizazi Changu’ mradi ambao umelenga kuboresha afya kwa wanawake wajawazito na watoto nchini Tanzania ambao utasaidia kupunguza vifo kwa mama na mtoto.

Aidha ukiachilia mbali kupunguza vifo kwa mama na mtoto mradi huo pia umelenga kuongeza ufahamu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu pamoja na kukusanya fedha kusaidia vifaa vya matibabu na kutoa bima kwa watoto wenyeuhitaji.

Ikumbukwe kuwa Shindano la Urembo la Dunia la 71 ambalo limeanza Februari 18, 2024 linatarajia kutamatika Machi 9, 2024.