Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hiki ndicho kiungo cha mwili kinachomtesa Beyonce

Muktasari:

  • Wengi wanaweza kudhani ni mtindo wake wa fashion kuweka nywele ndefu zenye kufunika masikio na kuvaa hereni nyingi na kubwa, lakini ukweli ni kwamba nyota huyo hutumia mtindo huo kuficha masikio yake.

Marekani. Ni ngumu kutaja orodha ya wasanii wakike wakubwa duniani na kuliacha jina la malkia wa pop Beyonce. Lakini licha ya umaarufu na mafanikio yake nyota huyo amekuwa akikosa amani kutokana na mwonekano wa masikio yake anayodai kuwa ni makubwa.

                        

Wengi wanaweza kudhani ni mtindo wake wa fashion kuweka nywele ndefu zenye kufunika masikio na kuvaa hereni nyingi na kubwa, lakini ukweli ni kwamba nyota huyo hutumia mtindo huo kuficha masikio yake.

                        

Anaamini uchaguzi wa hereni kubwa na nyingi ni njia ya kuwafanya watu wasizingatie masikio yake badala yake washangae muundo wa hereni.

Katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya na ITVX alipoulizwa sehemu zipi za mwili wake anatamani kuziboresha, nyota huyo alitaja miguu na masikio.

                   

"Kama ningeweza kubadilisha sehemu moja, ingekuwa miguu yangu. Baada ya miaka yote ya kucheza, imechoka kidogo. Na ninavaa hereni kubwa kwa sababu sipendi masikio yangu,"alisema Beyonce katika mahojiano yake hayo.