Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hamisa Mobetto abariki Aziz Ki kuoa mke wa pili

MOB 04

Muktasari:

  • Yamesemwa mengi kuhusu wawili hao baada ya ndoa, wakitabiriwa kuachana kwani mastaa huwa hawadumu. 

Dar es Salaam. Ni miezi saba sasa tangu Hamisa Mobetto na Stephane Aziz Ki wafunge ndoa. Baada ya hapo, nyota huyo wa zamani wa Yanga alitimkia Morocco kujiunga na Wydad huku akisindikizwa na mkewe ambaye baadaye alirejea nchini. 

Yamesemwa mengi kuhusu wawili hao baada ya ndoa, wakitabiriwa kuachana kwani mastaa huwa hawadumu. Hata hivyo, Mwananchi lilimsaka Hamisa na kupiga naye stori kuhusu maisha yake ya ndoa na nini mashabiki wao wanatakiwa kujua na kuachana na mambo ya mtandaoni.

MOB 04

Mwananchi: Kwanza hongera kwa kuendelea kupata dili za ubalozi.

Hamisa: Asante sana, hii ni kuonyesha mume wangu Azizi KI amenizidishia baraka baada ya kufunga ndoa. Hakika ni bonge la bwana kwangu.


Mwananchi: He kumbe ndoa yenu bado inapumua tofauti na tulivyosikia mitandaoni kuwa kuna tatizo la kuweza kuvunjika? Hongera sana kuwa bado upo upo kwa ndoa yako.

Hamisa: Sisi wenyewe tuliposoma mitandaoni tulishtushwa kama wewe hapo, yaani kuna baadhi ya watu wapo kutamani sana mimi kuachana na Aziz KI, ila nawaambia tu wachukue viti wakae maana watasubiri sana hilo. Pia waache kupenda kuchokonoa ndoa yangu mimi na mume wangu hatuachani ng'oo. Nimeolewa na mwanamume ninayempenda,

MOB 01

Mwananchi: Kuna sehemu niliona umesema hakuna kitu kimebadilika kwenye ndoa hii ulikuwa unamaanisha nini?

Hamisa: Okay, bora umeniuliza hili, maana wengi wameshangazwa mimi kusema hivi. Hii nilikuwa namaanisha tulivyoanza uhusiano na mume wangu Azizi KI na kwenye ndoa yanaendelea vile vile kitu kikubwa ni namheshimu sana na kumjali na kusapotiana kwa kila jambo, ndio maana nasema hakuna kitu kikubwa ambacho kimebadilika zaidi ya neno mke na mume.


Mwananchi: Zile habari za wewe kuhama kuishabikia  Simba na sasa unaishabikia Yanga ni za uongo?

Hamisa: Weeeee (Kicheko) hakuna kitu kipya bana hazijabadilika, kwanza lini mimi nilitangaza shabiki wa yanga? au kuihama Simba? Tusubiri msimu uanze itajulikana tu, watu wasiniongelee ni mapema mno.

MOB 02

Mwananchi: Utaenda kuishi anapofanya kazi Aziz KI?

Hamisa: Hapana hatuishi wote, ila nitakuwa naenda na kurudi na wala sijutii hili kwani nilikubaliana na hali nilipokubali kuolewa na mcheza mpira, hivyo nilijipanga kisaikolojia mapema kabla sijaingia kwenye ndoa.


Mwananchi: Hivi akitokea Aziz KI anataka kuoa mke wa pili utakubali?

Hamisa: Sina tatizo mume wangu akioa mke wa pili, jamani dini yetu ya Kiislamu inaruhusu ndoa za wake wengi, sasa mimi nitaweka pingamizi kwa nini ikiwa mume wangu ataona hitaji la kuongeza mke mwingine. Katika Uislamu, mwanamume anaruhusiwa kuwa na wake hadi wanne, mradi tu anawatendea kwa usawa katika masuala ya kifedha, mipango ya maisha na majukumu mengine chini ya uangalizi wake.


Mwananchi: Hivi huwa unapika? Maana ndoa za mastaa wengi hudaiwa kuvunjika sababu ya kushindwa kuingia jikoni kumpikia mme.

Hamisa: Kitu ambacho wengi hawakijui mimi napenda sana kupika na najua kupika, hivyo chakula cha mume wangu huwa namwandalia mwenyewe.

MOB 03

Mwananchi: Aziz KI anapendelea chakula gani?

Hamisa: Anapenda sana vyakula vya kitanzania, hasa ugali na mboga za majani hasa tembele.


Mwananchi: Unazungumziaje EX wako Kelvin kudaiwa kutoka na Lulu Diva?

Hamisa: Sina cha kuzungumzia lolote kuhusu yaliyopita, mimi ni mke wa mtu jamani.


Mwananchi: Unadhani ni sahihi wanao kuwaposti kwenye mitandao ya kijamii, je, huwa unawafundisha nini?

Hamisa: Huwa ninawafundisha kuwa na heshima na hasa kuwaheshimu watu wakubwa na wadogo wenzao nimewajenga pia kwenye makuzi ya kujiamini na kuwa imara.