Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Filamu yenye mapito ya Celine Dion mbioni kuachiwa

Muktasari:

  • Ikumbukwe kuwa Desemba 2022, Celine Dion alitangaza kuwa na ugonjwa adimu ambao hauna tiba kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akilazimika kughairisha ziara zake za muziki.

Mwanamuziki Celine Dion amezua gumzo mitandaoni baada ya trela ya filamu yake ikimuonyesha akilia kwa uchungu wakati akielezea mapito yake kufuatia na ugonjwa unaomsumbua wa ‘Stiff Person Syndrome’ ulioanza kumsumbua mwaka 2022.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘The Sun’ imeeleza kuwa licha ya Dion kujipa mapumziko ya muda lakini alikuwa akishirikiana na Amazon kurekodi filamu yake iitwayo ‘I Am: Celine Dion’ inayotarajiwa kutoka Juni 25 mwaka huu.

"Nimegundulika kuwa nina ugonjwa wa neva na sikuwa tayari kusema chochote hapo awali lakini niko tayari sasa.

"Siyo ngumu kufanya onesho, ni ngumu kughairi onesho, alisema huku akitokwa na machozi, ninafanya kazi kwa bidii kila siku lakini lazima nikubali, imekuwa ngumu, nimewakosea sana watu, ikiwa siwezi kukimbia nitatembea. Ikiwa siwezi kutembea, nitatambaa lakini sitaacha, kufanya ninacho kipenda,” amesema.

Ikumbukwe kuwa Desemba 2022, Celine Dion alitangaza kuwa na ugonjwa adimu ambao hauna tiba kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akilazimika kughairisha ziara zake za muziki.

Filamu hiyo ni njia ya kuonesha vita yake na ugonjwa huo ambao haujulikani sana kwa umma, kulingana na tangazo la Amazon, filamu itafichua yale yote yaliyokuwa nyuma ya pazia wakati wa mapambano ya kutafuta tiba ya ugonjwa huo.