Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Drake Kendrick Lamar kufikia ya Tupac na B.I.G?

Muktasari:

  • Utakumbuka Dame Dash, Jay Z na Kareem ‘Biggs’ Burke ndiyo walianzisha Roc-A-Fella Records mwaka 1995 na kuwasaini Kanye West, Cam’ron na Jadakiss, kabla ya kuiuza kwa Universal Music Group (UMG), kampuni mama ya Def Jam Recordings.

Wakati Drake na Kendrick Lamar wakiendeleza vita vya maneno katika ulimwengu wa Hip Hop, Dame Dash amezungumzia jinsi hali ilivyokuwa kipindi Jay Z na Nas wanashughulikiana katika nyimbo zao.

Utakumbuka Dame Dash, Jay Z na Kareem ‘Biggs’ Burke ndiyo walianzisha Roc-A-Fella Records mwaka 1995 na kuwasaini Kanye West, Cam’ron na Jadakiss, kabla ya kuiuza kwa Universal Music Group (UMG), kampuni mama ya Def Jam Recordings.

Akizungumza katika Podcast ya Moguls In The Making, Dame amesema licha ya Jay Z na Nas kushambuliana sana katika nyimbo zao, hawakuwa na wasiwasi wa kuibuka vurugu kama inavyotaka kuwa kati ya Drake na Kendrick Lamar.

“Hakukuwa na hofu ya sisi kuumia wala kutokea vurugu yoyote. Hakukuwa na hofu iliyotujia kuhusu vita yoyote tuliyokuwa nayo linapokuja suala la vurugu, kamwe hatukuwa na wasiwasi wa jambo kama hilo.” alisema Dame.

Dame anatazama mvutano wa Drake na Kendrick Lamar kama ilivyokuwa kwa The Notorious B.I.G na Tupac miaka ya 1990 hadi kupelekea mauaji yao na kusema hiyo ni mbaya zaidi katika utamaduni ya Hip-hop.

“Sasa, Pac na B.IG ni kama waliuawa, lakini ni kama unauawa katika Hip-Hop. Walipambana halafu wakaishia kufa, sasa hii ni mbaya zaidi.” alisema Dam Dash.

Ingawa hadi sasa siyo Drake wala Kendrick Lamar waliyepata madhara yoyote kimwili kutokana na mvutano wao, kulikuwa na uvumi kwamba risasi chache vilizofyatuliwa baadhi ya maeneo ya wasanii hao vinahusisha ugomvi wao.

Mathalani ni tukio la mlinzi kupigwa risasi nje ya jumba la kifahari la Drake, ingawa hakujawa na uthibitisho wowote ikiwa tukio hilo ni la bahati mbaya au laa, ugomvi wa Drake na Lamar umehusishwa kwa kiasi kikubwa.

Ikumbukwe ugomvi kati ya Jay Z na Nas ambao Dash kauzungumzia, ulianza baada ya Nas na wenzake kukubali kushiriki katika albamu ya kwanza ya Jay Z, Reasonable Doubt (1996), kisha lebo yake, Roc-A-Fella Records italisaini kundi lao la The Firm.

Hata hivyo, Nas na wenzake walipiga chini kimya kimya makubaliano hayo na kusaini Aftermath Entertainment ya Dr. Dre ndipo ugomvi ukaanza.

Jay Z alimchana Nas kupitia wimbo ‘Takeover’, Nas alijibu kupitia ‘Ether’, kitu kilichomfanya Hov kurejea studio na kuachia ‘Supa Ugly’, ngoma ambayo Dam Dash katika mahojiano yake na Moguls In The Making, anasema haikuipenda hata kidogo.

Hii vita ilikuja baada ya kumalizika ugomvi wa Tupac na B.I.G kufuatiaa vifo vyao kati ya mwaka 1996 na 1997. Wawili hao walikuwa katika vita vilivyokuwa vinaendelea kati ya East Coast na West Coast.

Tupac mzaliwa wa New York aliwakilisha East Coast baada ya kusaini Death Row Records yenye makao Los Angeles, mara nyingi alirushiana maneno na wenyeji wa New York, B.I.G na Diddy kutoka West Coast akiwakilisha Bad Boy Records ya New York.

Vita vya maneno katika nyimbo zao vilichukua nafasi na kufikia hatua mbaya, Tupac alitoa wimbo ‘Hit ‘Em Up’ ambao ulimlenga B.I.G ambaye alijibu mapigo kwa kuachia ‘Who Shot Ya?’ uliokuwa na maneno mengi ya dhihaka ingawa alikanusha kumlenga Tupac.