Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Drake afuta ngoma aliyotumia sauti ya Tupac

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa tovuti ya Billboard, imeeleza kuwa ilifuatilia platform zote za kusikiliza wimbo huo na kugundua kuwa ngoma hiyo tayari imefutwa siku ya jana Alhamisi Aprili 25.

Baada ya mwanasheria wa familia ya Tupac, Howard King kumpa saa 24 rapa Drake kufuta ngoma ya‘ Taylor Made Freestyle’ aliyotumia AI (akili bandia), kutengeneza sauti ya marehemu Tupac, hatimaye mwanamuziki huyo kutoka Canada tayari amefuta wimbo huo kwenye platform za kusikiliza muziki.

Kwa mujibu wa tovuti ya Billboard, imeeleza kuwa ilifuatilia platform zote za kusikiliza wimbo huo na kugundua kuwa ngoma hiyo tayari imefutwa siku ya jana Alhamisi Aprili 25.

Kupitia taarifa iliyotolewa na mwanasheria huyo ilieleza kuwa siyo uungwana kutumia sauti ya marehemu bila idhini ya familia yake huku akiweka wazi kuwa huu ni unyanyasaji wa wazi kwa moja wa nguli katika muziki wa Hip-hop.

"Taylor Made Freestyle’ ni wimbo ambao Drake aliuachia rasmi kwa ajili ya kumchana Kendrick Lamar ambapo alitumia AI kutengeneza sauti ya marehemu Tupac na Snoop Dogg wimbo huo ukiwa kama ni muendelezo wa bifu lao.

Tupac Shakur alizaliwa Juni 16, 1971 na alifariki Septemba 13, 1996 akiwa na miaka 25, huku kesi ya mauaji ya kifo chake bado inaendelea mahakamani.