Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond aomba Arena iwepo Tanzania

Muktasari:

  • Diamond ameyasema hayo leo Februari 26,2025 wakati akiingia kwenye tuzo za muziki za Trace zinazofanyika Zanzibar Kisiwani Unguja

Zanzibar. Staa wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameiomba Serikali kutengeneza Arena kwa ajili ya matamasha makubwa ya muziki kama Trace.

Diamond ameyasema hayo Februari 26,2025, wakati akiingia kwenye tuzo za muziki za Trace zilizofanyika Zanzibar Kisiwani Unguja.

“Imagine Arusha kunatengenezwa uwanja mwingine. Tungepata Arena na sisi ingetusaidia, hizi event zikifanyika nyingi zinatukuza. Wasanii wa Kitanzania tumejitahidi sana kuweka nguvu ya kisanaa ambayo inaonekana.

"Kwa hiyo tunaomba serikali ituunge mkono kwenye kutuwekea Arena. Na itasaidia vitu vingi, Basketball, Netball, kutafanyika mikutano na mambo mbalimbali. Sanaa ya Tanzania ni kubwa sana lakini kwa sababu tunakosa vitu kama Arena unakuta watu wanaenda kwenye nchi za watu wengine,” amesema Diamond.

Aidha nyota huyo wa muziki ameongezea kwa kutolea mfano nchini Rwanda wanavyonufaika na Arena zao.

"Mimi msanii naongea na Basata kila siku lakini sitaki kuamini kama fedha hamna ni kuamua tu naamini Dk Samia Suluhu Hassan ni mtu ambaye ameleta mageuzi, katika vitengo tofauti tunamuomba na sisi kama wasanii atutengenezee Arena,” amesema Diamond.

Licha ya Diamond kutoa ombi hilo, Februari 22, 2025 katika Tuzo za Wachekeshaji nchini Rais Samia Suluhu Hassan aliweka wazi kuwa serikali ipo kwenye mpango wa kutengeneza Arena kwa ajili ya wasanii.

“Wasanii wa sanaa zote napenda mtambue kuwa serikali inawatambua. Inawathamini na inawaheshimu. Uwepo wangu hapa ni ahadi ya ushirikiano kwenu katika kuendeleza tasnia hii. Katika ziara ya Korea tulipata mkopo rahisi wa dola 2.5 bilioni na tukasema katika fungu hili lazima wasanii wafaidike.

"Na ndio ile aliyoisema waziri kwamba tunakwenda kujenga Arena ya aina yake, studio kubwa na Arena kwa ajili yenu wasanii wa aina zote. Tupo kwenye mazungumzo hatua za mwisho, kwa sababu wakikupa pesa yao wale inabidi uwaambie unaitumia kwenye 'field' gani na kwanini. Nadhani wametuelewa na wamekubali fedha iende huko,”alisema Rais Samia.

Aidha aliendelea kwa kusema Arena na studio kubwa zitajengwa kwa ajili ya kuwawezesha wasanii kufanya kazi zao kwa raha.

"Kwa hiyo wasanii wa aina zote imani yangu, mtatumia miundombinu hiyo. Tutaendelea kudhihirisha thamani yenu kwa kuendeleza sera rafiki zitakazokuza sanaa yenu ili vipawa vyenu viwanufaishe kiuchumi,” alisema Rais Samia. 

Utakumbuka Kigali, Rwanda tayari kuna Arena  iitwayo BK, yenye uwezo wa kuingiza watu 10,000.