Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

D Knob kama Nandy maisha ya muziki yamebadilisha ramani

Muktasari:

  • Miaka yake 11 akiwa katika biashara ya muziki, D Knob aliweza kutengeneza nyimbo za kuelimisha na kuburudisha huku mitazamo na mtindo wake wa maisha vikiwa na ushawishi kwa vijana wengi. Huyu ndiye D Knob

Dar es Salaam. Mwaka 1998 D Knob alianza muziki kwa kujifunza kupitia nyimbo za Tupac, miaka mitano baadaye jina lake likachomoza katika Bongo Fleva na kuwa miongoni mwa wachanaji wakali kuwahi kutokea.

Miaka yake 11 akiwa katika biashara ya muziki, D Knob aliweza kutengeneza nyimbo za kuelimisha na kuburudisha huku mitazamo na mtindo wake wa maisha vikiwa na ushawishi kwa vijana wengi. Huyu ndiye D Knob.

Wakati wimbo wa D Knob, Elimu Mitaani.com (2003) unatoka alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), kufanya vizuri kwa wimbo kulipelekea kuacha masomo maana alipata show nyingi ambazo kwa wakati huo zilimlipa vizuri.

Ukiachana na D Knob, msanii mwingine aliyeacha CBE baada ya kupata umaarufu kimuziki ni Nandy kufuatia kufanya vizuri katika shindano la Tecno Own The Stage nchini Nigeria na kupata Dola 15,000.

Mdundo wa wimbo huo uliotengenezwa na Miikka ‘Mwamba’ Kari, D Knob alikaa nao kwa zaidi ya mwaka mmoja akiufanyia mazoezi na kuandika mistari hadi alipokuja kufanikiwa kurekodi.

Hata hivyo, baada ya kurekodi hakuwa na fedha ya kushuti video, hivyo ikambidi amuandikie email Mikka Mwamba na kumuomba msaada, wakati huo Mikka alikuwa amesafiri kwenda kwao Finland.

Mikka Mwamba ambaye alifanya kazi FM studio kati ya mwaka 1999 hadi 2004, alimtumia D Knob fedha kiasi cha Sh100,000 ili kushuti video ya wimbo, Elimu Mitaani.com (2003) na ilipotoka ikamtambulisha vizuri.

Ikumbukwe Miikka Mwamba ametengeneza nyimbo maarufu Bongo kama Eno Maiki (Ziggy Dee), Babygal (Mad Ice), Kamanda (Daz Nundaz), Kwenye Chati (Balozi Dola Soul), Mkiwa (K Sal), Kitu Gani (D Knob), Maria Salome (Saida Karoli), Tamala (Hardmad) n.k.

Wakati ameachia wimbo, Elimu Mitaani.com (2003), D Knob alienda Clouds FM kujitambulisha kwa DJ Venture na Steve B maana walikuwa wanacheza sana ngoma hiyo bila kumjua msanii aliyeimba ni nani hasa.

DJ Venture na Steve B hawakumjua D Knob hadi alipojitambulisha kuwa yeye ndiye kaimba wimbo, Elimu Mitaani.com (2003). Basi kuanzia hapo wakaanza kufanya kazi pamoja, na DJ Steve B ndiye mtu wa kwanza kumpa D Knob show.

Mbali na D Knob, msanii mwingine aliyefanya kazi na DJ Steve B “DJ Skills” ambaye alifariki mwaka uliopita, ni Joslin, mkali huyo wa RnB, albamu zake mbili, ‘Perfume’ na ‘Umewezaje’ zote zilisimamiwa na DJ Steve B.

Wimbo wa D Knob, Nishike Mkono (2014), akimshirikisha Mwasiti ndio wa mwisho kwake kuachia na baada ya hapo akaacha muziki wa Bongofleva na kuamua kuokoka na hadi sasa anaishi maisha ya wokovu.

Kwa kipindi chote ambacho alikuwa katika tasnia, D Knob hakuwahi kushinda tuzo za muziki Tanzania (TMA) kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii waliofanya vizuri zaidi tangu kitambo akiwemo Dully Sykes na Mr. Blue.

Hadi anaamua kuacha muziki, D Knob alikuwa ametoa albamu mbili, Elimu Mitaani.com (2005) na Bomoa Mipango (2008). Hiyo ni sawa na K-Lynn ambaye aliachia muziki akiwa ametoa albamu mbili, Nalia kwa Furaha (2004) na Crazy Over You (2007).

Mdundo wa wimbo wa D Knob ‘Sauti ya Gharama’ ulikuwa kwa ajili ya kutumika kwenye wimbo wa Mh. Temba ‘Nampenda Yeye’ ila P-Funk Majani aliposikiliza kwa makini akaamua nyimbo hizo zibadilishane midundo na zilipotoa zote zikafanya vizuri.