Chiku wa Kombolela apata funzo

Muktasari:
- Chiku alisema kuwa, tofauti na muziki, uigizaji ulimlazimu kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kuheshimu muda, hiyo ilikuwa tofauti kubwa kwa mtu kama yeye aliyezoea kuwa katika tasnia ya muziki.
Dar es Salaam. Mwimbaji wa muziki wa taarabu, Hanifa Maulid ‘Jike la Chui’ anayetamba katika tamthilia ya Kombolela kwa jina la Chiku, amesema amejifunza mengi baada ya kupata nafasi ya kuigiza.
Chiku alisema kuwa, tofauti na muziki, uigizaji ulimlazimu kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kuheshimu muda, hiyo ilikuwa tofauti kubwa kwa mtu kama yeye aliyezoea kuwa katika tasnia ya muziki.
“Hii ni tamthilia yangu ya kwanza kabisa ya Kombolela, unajua nimezoea kuwa mwimbaji lakini katika tamthilia hii, si kuhusu wewe. Lazima uwe ‘saiti’ kwa wakati. Hii imenifundisha kuheshimu muda wa kijeshi na kufanya kazi kwa bidii. Sasa nawaheshimu sana waigizaji. Uvumilivu wao ni wa ajabu.” amesema Chiku.
Pia Chiku amekiri kuwa ingawa amekuwa akipenda muziki, ndoto ya kuigiza imekuwepo muda mrefu, lakini aliwahi kuwa na aibu ya kuigiza mbele ya kamera.
"Lakini hii ndiyo mara ya kwanza maishani mwangu niko mbele ya kamera na siimbi. Ilikuwa ya ajabu sana. Nimejifunza mengi kutoka kwa kila mtu, siyo tu mastaa,," amesema Chiku.