Mataji ya Yanga yamchizisha Konde Boy

Muktasari:
- Harmonize ambaye ni shabiki wa Yanga, ameliambia Mwananchi, anajiona mwenye bahati kwa kuishabikia timu yenye kubeba makombe kila uchao.
Dar es Salaam. Staa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Harmonize a.k.a Konde Boy, amefunguka kwamba ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho iliyotwaa Yanga msimu huu vimempa furaha kubwa kwani, kulikuwa na kelele na hila nyingi kabla ya msimu wa 2024-2025 kufikia tamati.
Harmonize ambaye ni shabiki wa Yanga, ameiambia Mwananchi, anajiona mwenye bahati kwa kuishabikia timu yenye kubeba makombe kila uchao.
“Najiona ni mtu mwenye bahati sana kuishabikia hii klabu yenye kubeba makombe kila kukicha. Najiona ni mwenye bahati sana kuishi kwenye hii karne nakuweza kuiona Yanga SC noma kuliko Yanga ya msimu wowote,” amesema Harmonize na kuongeza;
“Kuna muda huwa nawaza hawa wenzangu wanaoshabikia timu nyingine walikua wapi kipindi sisi tunafanya chaguzi? Ndipo nagundua kwanini huwa wanapata maradhi kama vile pressure, kisukari na magonjwa mengine,” alitania.