Ben Pol hana takwimu za kazi zake

Msanii Ben Pol amesema kuwa ni wakati wa kampuni zinazofanya biashara ya miito ya simu ya nyimbo za wasanii wa muziki wa hapa nyumbani kuacha kufikiria kuwa wasanii siku hizi hawajitambui.
Ben Pol alisema pamoja na kwamba yeye ni moja ya wasanii ambaye ana nyimbo zinazotamba kama 'Pete', 'Samboira', 'Number one fan', 'Nikikupata', lakini mpaka leo hana takwimu ya watu ambao wamenunua kazi zake.
Anasema kuwa hivi sasa wasanii wanasoma na wana taaluma zao wanajua wanafanya nini kwenye muziki na si kwamba mtu hana kazi ndo kwa maana anafanya muziki.
Alisema pia ni vizuri serikali ikaingilia suala hilo ili wasanii wapate haki yao.