Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

A to Z ufunguzi wa ZIFF ulivyofana 2024

Muktasari:

  • Katikati ya sherehe hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF, Joseph Mwale, alitoa wito wa kwa wahisani wa ndani kusaidia kuhakikisha mafanikio na ustawi wa tamasha hilo kwa siku zijazo

Zanzibar. Tamasha la 27 la Zanzibar International Film Festival (ZIFF) limefunguliwa leo Agosti Mosi, limeanza kwa sherehe zilizofana katika Viwanja vya Stone Town, huku likiwa na burudani ya kusisimua kutoka kwa Wamwiduka Band. 

                      

Wamwiduka Band wakitumbuiza kwenye tamasha la ZIFF

Katikati ya sherehe hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF, Joseph Mwale, alitoa wito wa kwa wahisani wa ndani kusaidia kuhakikisha mafanikio na ustawi wa tamasha hilo kwa siku zijazo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mwale alisisitiza umuhimu wa tamasha hilo, siyo tu kama tukio la burudani bali pia kama msingi wa kitamaduni kwa Zanzibar na nje ya mipaka yake.

                

Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF, Joseph Mwale akihutubia kwenye tamasha hilo

"ZIFF siyo tukio tu, ni uhai kwa serikali yetu, jamii yetu, na kila mtu anayethamini sanaa," alisema Mwale, akisisitiza jukumu la tamasha hilo katika kukuza tamaduni na sanaa.

Mwale alionesha wasiwasi wake juu ya kushuka kwa kasi kwa tamasha hilo huku akisisitiza umuhimu wa kuifufua ZIFF. 

"Hili ni tamasha la ndani ambalo sasa linategemea msaada wa ndani. Tukiacha kuchukua hatua sasa, tunaweza kuamka siku moja na kulikosa. Hatuwezi kumlaumu mtu yeyote isipokuwa sisi wenyewe,"alisema

Kutokana na hayo Mwale alihimiza kila mtu kuchukua jukumu la kulitunza.

"Usisubiri kuulizwa ulikuwa wapi ZIFF ilipoporomoka. Ni wakati wa kufufua," alisisitiza huku akionesha kuwa zinahitajika juhudi za pamoja zinazohitajika ili kuhakikisha tamasha hilo linaendelea kukua.

"Tufanye kazi pamoja kuhakikisha kwamba tamasha hili siyo tu linadumu bali linastawi, likiendelea kuwahamasisha vizazi vijavyo kuungana," alimalizia 

Hata hivyo baada ya Mwale kushuka jukwaani hapo alipanda Emilio Rossetti ambaye ni Balozi Msaidizi Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania alisisitiza imani kuu tatu za Umoja wa Ulaya kuhusu utamaduni.

                       

Emilio Rossetti ambaye ni Balozi Msaidizi Umoja wa Ulaya (EU)  akihutubia kwenye tamasha hilo

Kwanza, Umoja wa Ulaya unathamini utamaduni kama njia ya kuchochea mazungumzo na kukuza mahusiano ya kiutamaduni. Umoja wa Ulaya uko tayari kushirikiana na sanaa za Afrika.

Pili, Umoja wa Ulaya umejidhatiti kulinda urithi na utambulisho, dhidi ya athari mbaya za kampeni za upotoshaji ambazo husababisha migogoro ya kiutamaduni. Kama muungano wa mataifa mbalimbali, Umoja wa Ulaya unasaidia uhifadhi wa utambulisho wa kitamaduni.

Mwisho, Umoja wa Ulaya unaona utamaduni kama nguvu inayochochea sekta za ubunifu, ikichangia maendeleo na ukuaji wa pamoja. Umoja wa Ulaya unaamini katika kukuza wasanii.

Kisha akapanda Mwenyekiti wa Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Chande Omar na kueleza kuwa ZIFF itawasukuma wasanii kucheza na kutunga filamu zinazohusu changamoto za jamii na siyo mapenzi tu.

                      

Mwenyekiti wa Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Chande Omar akihutubia kwenye tamasha hilo

"Tunatarajia katika tamasha linalokuja mwakani tufanye kazi karibu na Serikali hii kutokana na jambo moja tunakusudia kuwasukuma wasanii wa filamu kutengeneza filamu zinazohusu changamoto zilizopo kwenye jamii yetu hivi sasa.

Baada ya kumalizika kwa hotuba ya kiongozi huyo maonesho ya filamu ambazo hazijawahi kuoneshwa sehemu yoyote yalianza.