Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Mtasubiri’ ya Diamond na Zuchu yapigwa marufuku

Muktasari:

  • Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepiga marufuku vyombo vya utangazaji na mitandao ya kijamii kutoonyesha wimbo wa ‘Mtasubiri’ ulioimbwa na msanii Nasib Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz akimshirikisha msanii mwenzake Zuhura Othman (Zuchu).


Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepiga marufuku vyombo vya utangazaji na mitandao ya kijamii kutoonyesha wimbo wa ‘Mtasubiri’ ulioimbwa na msanii Nasib Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz akimshirikisha msanii mwenzake Zuhura Othman (Zuchu).

Video hiyo iliyotoka mwezi mmoja uliopita mpaka sasa imeshatazamwa na watu zaidi ya milioni 10 kwenye mtandao wa Youtube na ni moja kati ya nyimbo zilizoko katika albamu fupi (EP)  ya First of All (FOA) ukiwa wimbo namba nne.

Kuzuiwa kwa video hiyo kumetangazwa kupitia taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuthibitishwa na Meneja  wa huduma za utangazaji, Mhandisi Andrew Kisaka, alipozungumza na Mwananchi Digital.

Hata hivyo, alisita kutoa maelezo zaidi akitaka yatolewe na Baraza la Sanaa la Taifa(Basata).

“Ni kweli hiyo ni taarifa yetu, lakini kwa maelezo zaidi watafute Basata kwani wao kiutaratibu ndio wanaleta maombi na sisi tunachofanya ni utekelezaji kama wasimamizi wa vyombo vya utangazaji,” amesema Mhandisi Kisaka.

Katika tangazo hilo linaloonyesha limetolewa Aprili 29, 2022 likiwa na kichwa cha habari vyombo vya utangazaji kutopiga wimbo wa wasanii hao.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa TCRA imepokea taarifa kutoka Basata ya kuzuia usambazaji wa video ya wimbo wa wasanii hao unaopigwa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya utangazaji.

Imesema sababu za kuzuia video hiyo ni kutokana na kuwa na kipande kinaonyesha wahusika wapo kanisani wanaimba kwaya lakini baadae wakaacha na kuelekea kwingine.

“Kipande hicho cha video kimeleta ukakasi miongoni mwa waumini wa madhehebu ya dini na kuleta hisia kwamba ni dharau juu ya dini/madhehebu fulani.

“Hivyo kwa barua hii, TCRA inaagiza vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii hapa nchini kutorusha video ya wimbo uitwao’Mtasubiri,” imesema sehemu ya barua ikiongeza kuwa wimbo huo utarejeshwa kipande hicho kitakaporekebishwa.

Mwananchi Digital iliutafuta uongozi wa WCB, ambapo Meneja wa lebo hiyo, Hamis Tale, alijibu kwa ujumbe mfupi; “sijui mie.”

Basata walipotafutwa kupata maelezo zaidi, namba ya Katibu Mkuu wake, Mniko Mtiko iliita bila ya kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi kupitia WhatsApp ya kutaka ufafanuzi kuhusu jambo hilo hakujibu.

TCRA inatangaza kufungia video hiyo ikiwa imepita miaka minne tangu ilipofungia nyimbo 15 na kati ya hizo mbili zilikuwa za Diamond ikiwemo Wakawaka na Hallelujah.

Nyingine ilikuwa ni na kwenye mabano jina la msanii Kibamia (Roma Mkatoliki), Pale Kati patamu na Maku Makuz (Ney wa Mitego), Hainaga Ushemeji) Manifongo), I am Sorry JK (Nikki Mbishi.

Pia ilikuwepo Chura) na Nimevurugwa (Snura), Tema mate tumchape (Madee), Uzuri wako (Jux), Nampa papa (Gigy Money) na Nampaga(Baranaba).