Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Othman azungumzia miaka 62 ya Muungano

Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo, Othman Masoud Othman ‘OMO’

Muktasari:

  • Othman ambaye amewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa visiwa amesema hayo leo Jumapili, Aprili 26, 2026 wakati akifungua kongamano la vijana visiwani Pemba.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo, Othman Masoud Othman ‘OMO’ amehoji faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa uchumi wa kisiwa hicho.

Othman ambaye amewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa visiwa amesema hayo leo Jumapili, Aprili 26, 2026 wakati akifungua kongamano la vijana visiwani Pemba.

Kongamano hilo lilikuwa na mada uchumi wa Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanganyika uliofanyika Aprili 26, 1964.

Mwenyekiti huyo amezungumzia uchumi wa Zanzibar kutowezesha bidhaa nyingi kuzalishwa visiwani huko akisema zinaagizwa kutoka nje.

Amesema bajeti ya Serikali ya Zanzibar ni Sh5.1 trilioni lakini nchi hiyo kwa kutumia mapato ya ndani ina uwezo wa kupata Sh2.2 trilioni na Sh2.9 trilioni ni mikopo kutoka kwenye benki  ambazo hukopewa na Serikali ya Muungano.

Kwa mwaka 2025/26 amesema Serikali ya Zanzibar ilipanga kutumia bajeti ya Sh6.9 trilioni na ikabidi ikope nyingine na mapato yake ya ndani ni Sh2.3 trilioni, kitendo kinachoilazimu nchi hiyo kuingia kwenye mikopo ndani na nje ya nchi.

“Takribani Sh1 trilioni inakwenda kulipa mishahara, jambo zuri zaidi mwaka huu utakaoanza kesho kutwa 2026/27 Serikali inakusudia kwenda kutumia Sh8.1 trilioni na vyanzo vyote vya mapato ya ndani ni Sh3.9 trilioni lakini wanakwenda kukopa kwenye taasisi za ndani za fedha ambazo riba ni kubwa na muda wa kukopa ni mdogo,” amesema.

Pamoja na hayo amesema Serikali haijabuni vyanzo vipya vya mapato badala yake imeongeza ushuru kwa wananchi ikiwamo kwenye shisha na pipi.

Ushuru mwingine alioutaja ni kwenye magari yanayoingizwa nchini, tozo za barabara na mafuta akisisitiza tozo hizo ni nyingi kwa wananchi.

“Tatizo liko wapi, mimi nasema hakuna nchi inafanyabiashara hasa kwa nchi ambayo haina rasilimali, Zanzibar haina mafuta haina gesi, dhahabu, almasi wala madini yeyote,” amesema. 

Othman amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuzingatia haki za kila nchi kuendelea na haki zake na kila mmoja kufaidika.

Sababu ya kusema hivyo, amesema chini ya Muungano umeunganishwa kwa ujanja kwa madhumuni ya mmoja kudhibitiwa.

Makamu Mwenyekiti wa Ngombe ya Vijana ACT Wazalendo, Nassor Ahmed amesema kwa miaka 60 Zanzibar ipo kwenye janga na kiuchumi haipigi hatua na inarudi nyuma kiuchumi.

Amesema sio kwamba wanachuki na Muungano bali wanautaka wenye haki na usawa.

Mwanasheria Mkuu wa ACT- Wazalendo Omar Said Shaaban amesema tofauti na matarajio ya wengi kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ungewanufaisha.

 “Pale inapoonekana Zanzibar inataka kufanya jambo Fulani linasemwa ni jambo la Muungano au la kikatiba,utatuzi unaosemwa ni wa kero za muungano hautatui mambo ya msingi.