Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hali ya hewa yakwamisha mapokezi ya ndege mpya Zanzibar

Muktasari:

  • Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais Ikulu Zanzibar, zimeomba radhi kutokana na mabadiliko ya ratiba za ujio wa ndege mpya aina ya Boeing B8787- Dreamliner iliyotokana na hali ya hewa.

Unguja. Ndege mpya aina ya Boeing B8787- Dreamliner iliyokuwa inatarajiwa kupokewa leo Jumatatu Agosti 19, 2024, imekwama.

Kwa mujibu ratiba iliyokuwa imetolewa, ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 262 ilikuwa ikitarajiwa kutua saa 10:00 jioni kisiwani humo na kupokelewa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanzibar.

Taarifa ilitolewa leo Agosti 19, 2024 kwa vyombo vya habari na kitengo cha uhusiano na mawasiliano, kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesema mabadiliko hayo yamesababishwa na changamoto ya hali ya hewa ambayo ipo nje ya uwezo.

"Hivyo imesababisha kubadilisha ratiba ya safari, ratiba nyingine mpya ya kuwasili kwa ndege hiyo itatolewa, Kampuni ya Ndege Tanzania inaomba radhi," imesema sehemu ya taarifa hiyo,"

Pia taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Raqey Mohamed, imesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 262 na awali zilikuwa mbili, hivyo kuwasili kwake itaongeza idadi na kuwa tatu za aina hiyo.

Akizungumza na Mwananchi, Raqey amesema hali ya hewa iliyobadilika ni ya Marekani iliponunuliwa Ndege hiyo.