Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT yaingilia kati kupanda bei ya mafuta

Kaimu Naibu katibu mkuu ACT-Wazalendo Zanzibar, Salim Abdalla Biman akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisi za chama hicho Vuga mjini Unguja. Picha na Muhammed Khamis

Muktasari:

  • Wamesema kuna haja Serikali kutizama kwa makini ongezeko la bei ya mafuta na kutafuta mbinu ya kuwapunguzia makali wananchi.

Unguja. Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufanya mapitio ya mfumo wa uliopo wa uingizaji mafuta ya jumla ambao wanadaia umekua na ukiritimba na kusababisha kupanda kwa bei kila mwezi.

Kauli hiyo imesemwa leo November 12 na Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Salim Bimani kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Amesema mfumo uliopo sasa unapunguza ushindani na uwezekano wa kutumika vibaya na muagizaji mmoja pekee.

Amesema kuna haja Serikali kuangalia upya mfumo wa kodi za Serikali katika sekta ya nishati na mafuta nchini ili kuweka unafuu kwa wananchi. 

Akitolea mfano amesema katika miaka ya nyuma kulikuwa na sera maalum ya kudhibiti bei ya mafuta ya taa kwa kuyaondolea kodi zote inapobidi.

Pia ameitaka Serikali ya kutazama upya gharama za uingizaji wa mafuta kutoka katika bandari ya Dar es Salaam kuja bandari ya Zanzibar, kuna uwezekano mkubwa kuwapunguzia wananchi mzigo huu mkubwa ambao wanaubeba.

Pamoja na hayo amesema kuna haja kuwa na sehemu ya kuhifadhia mafuta kwa dharura yaani (Strategic Fuel Reserve Facility) ili kuruhusu mfumo wa kuagiza mafuta angalau kwa miezi mitatu ili kuondosha utaratibu huu wa kupandisha bei ya mafuta kiholela.

"Kila baada ya mwezi, bei mpya inatolewa utaratibu huu unaharibu kabisa mipango na bajeti na mipango ya wafanyabiashara na wananchi ambazo wanajiwekea kutumia katika mwezi husika," amesema.

Katika hatua nyengine alizungumzia kuhusu kuwepo kwa matenki ya mafuta eneo la mtoni na kueleza kuwa yalijengwa maalumu kuhifadhi mafuta mengi zaidi lakini cha ajabu yamekodishwa wa watu binafsi.

Aidha wameitaka Serikali kupunguza matumizi yasiokua ya lazima, ikiwemo magari mengi ili kufidia gharama ya ongezeko bei ya mafuta.

Huku hayo yakijiri Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hamza Hassan Juma amesema Serikali kwa muda mrefu wamekua na utaratibu wa kufidia sehemu ya gharama kwenye bei ya mafuta.

Amesema kupanda na kushukwa kwa mafuta ni jambo ambalo haliwezi kuepukika kwani ni matokeo ya kidunia.

Kuhusu kuwa na sehemu maalumu ya kuhifadhi mafuta amesema Serikali ina dhamira hiyo na ndiyo maana wameshatenga eneo Mangapwani ambako kutakua na bandari maalumu ya mafuta.