Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunukiwa udaktari wa heshima (PhD) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  

Mkuu huyo wa nchi ametunukiwa udaktari huo leo Jumatano Novemba 30, 2022 na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Jakaya Kikwete katika mahafali ya 52 ya chuo hicho yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.