Dk William Ruto ameapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Kenya leo Jumanne, Septemba 13, 2022 katika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Ruto ameapishwa na Jaji Mkuu Martha Koome kuchukua nafasi ya Uhuru Kenyatta, ambaye amemaliza muda wake wa utawala wa miaka kumi aliyoianza Aprili 9, 2013, akivaa viatu vya Mwai Kibaki.