Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vyombo vya habari Pakistan vyafunguka

Vyombo vya habari nchini Pakistan vimetoa tamko la kulaani mahakama ya kupambana na ugaidi kuwahukumu kifungo cha maisha jela baadhi ya waandishi wa habari wakiwemo walioripoti tukio la kukamatwa na kushtakiwa kwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Imran Khan mwaka 2023.

Wakizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo wamesema  kilichofanyika ni kuminya uhuru wa vyombo vya habari, huku wakihoji sababu za watu kuhukumiwa bila kuwepo mahakamani.

‘’Hukumu iliyotolewa kwa waandishi wa habari na wachambuzi ni hatua kali sana. Inaweza kuwa ukosoaji wao ulivuka mipaka lakini haikupaswa hukumu kuwa hiyo. Kwanza kesi kuendeshwa huku watuhumiwa wakiwa hawapo mahakamani inatisha zaidi,’’ inaeleza sehemu ya taarifa ya vyombo hivyo iliyosomwa na Rajid Khan.

Vimeeleza kuwa sheria ya kupambana na ugaidi ina vifungu kandamizi na kubainisha kuwa ndio vinatumika kuhukumu watu wa kada mbalimbali bila kuzingatia haki.

‘’Chini ya sheria ya kupambana na ugaidi mahakama zinaweza kuwashtaki watu wanaokwepa kesi bila uwepo wao mahakamani. Sisi tunaona kifungu hiki kinapotumika bila ulinzi unaofaa kinaweza kuwanyima washtakiwa haki za msingi za kujitetea na kupinga ushahidi,’’

‘’Katika yale matukio ya mwaka 2023 wengi wa waliohukumiwa walikuwa wakiishi nje ya nchi na hawakuhudhuria hata siku moja mahakamani. Hii inazua maswali mengi kuhusu uwazi na haki ya mchakato wa mahakama,’’alisema Khan.