Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utekaji wawaibua wanaharakati Pakistan

Utekaji wa watu katika baadhi ya maeneo nchini Pakistan umewaibua wanaharakati na kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka wakibainisha kuwa wanawake ndio wapo hatarini zaidi kwa sasa.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wanaharakati hao walisema utekaji huo mbali na kuibua hofu pia unatishia ukuaji wa uchumi kwani wakosoaji wa washauri wa mambo ya maendeleo pamoja na wawekezaji wanatishiwa.

"Baadhi ya wanawake nchini Pakistan wako katika hatari kubwa ya unyanyasaji wa kijinsia na utekaji. Ni kama tunaona hakuna wanaochukuliwa hatua kutokana na matukio haya na baadhi tunajua wanayoyafanya na tunawataja lakini hakuna kinachoendelea,’’ alisema Albert Patras, mwanaharakati wa haki za binadamu anayefanya kazi na wanawake walionusurika kutekwa kusini mwa mji wa Punjab.

Madai hayo yameibuka ikiwa umepita mwezi mmoja tangu tume ya pamoja ya Pakistan kukutana nchini Ubelgiji na kutoa mapendekezo kadhaa kuhusu malalamiko hayo.


Zainab Malik ambaye kitaaluma ni wakili, katika mkutano huo na waandishi wa habari alikosoa marekebisho ya 27 ya Katiba ya Pakistan, akieleza kuwa ndio chanzo cha  uvunjifu wa haki za binadamu nchini humo.

‘’Mabadiliko hayo yaliunda mahakama ya katiba ya shirikisho, kupanua udhibiti wa watendaji juu wa mahakama, kutoa kinga ya maisha yote kwa rais na uongozi wa kijeshi, na kuimarisha ushawishi wa jeshi,‘’

‘’Marekebisho haya yamevunja uhuru wa mahakama wa Pakistan na baadhi ya mambo yanayoendelea hata yakifika mahakamani sidhani kama kuna kitakachofanyika,’’alisema Zainab.