Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgombea udiwani aahidi mapinduzi kwenye kata yake

Mjumbe wa kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Adam Best Simba (kushoto) akimnadi mgombea udiwani kata ya Rau, Stallone Malinda

Muktasari:

  • Wananchi wa Rau wanahitaji kiongozi mwenye msukumo na uwezo wa kupigania maendeleo ya kweli badala ya siasa za maneno.

Moshi. Mgombea udiwani katika kata ya Rau kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Stallone Malinda ameahidi kusimamia ujenzi wa soko la kisasa kwenye kata hiyo hatua ambayo itachochea ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.

Akizungumza leo katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Rau Madukani, Malinda amesema wananchi wa Rau wanahitaji kiongozi mwenye msukumo na uwezo wa kupigania maendeleo ya kweli badala ya siasa za maneno.

“Nipeni nafasi ya kuwa diwani wenu. Nitahakikisha soko letu linapauliwa kisasa, linakuwa na vyoo, maji safi na huduma bora ili wafanyabiashara wetu wafanye kazi katika mazingira yaliyo bora na yenye staha,” amesema Malinda.

Aidha, ameeleza kuwa Zahanati ya Rau inakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa vifaatiba na wataalamu wa afya, hali inayowalazimu wakazi wa eneo hilo kwenda kutafuta huduma maeneo mengine na kuahidi kusimamia upatikanaji wa madaktari na vifaa ili wananchi wapate huduma karibu na makazi yao.

Katika sekta ya miundombinu, Malinda ametaja barabara za ndani zenye changamoto kubwa ikiwemo Kariwa Chini na Karikacha, ambazo hazipitiki nyakati za mvua.

“Nipeni nafasi ya udiwani nikajenge hoja katika baraza la madiwani ili kuhakikisha zahanati yetu ya Rau inaboreshwa na kuwekwa vifaatiba na wataalamu wa afya, ili kuwahakikishia upatikanaji wa huduma bora za afya,” amesema Malinda.

Ameongeza kuwa ataboresha barabara za ndani na kuhakikisha zinajengwa kwa kiwango cha lami. Nipeni nafasi mimi kijana wenu nikajenge hoja kwenye halmashauri ili kuleta maendeleo.”

Pia, ameahidi kushughulikia maboresho ya kituo cha polisi Rau ili kiwe na askari wa kudumu na mazingira bora ya kufanyia kazi, jambo ambalo amesema litaimarisha usalama wa wananchi na mali zao.

“Lakini pia nitahakikisha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vinapata mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kama ilivyoelekezwa na Serikali na walengwa mnaanzisha miradi ya kiuchumi,” amesema.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Adam Simba amesema hakuna sababu ya wananchi kuacha kumpigia kura Rais Samia Suluhu Hassan kwani Serikali yake imedhihirisha dhamira ya kweli katika kuboresha maisha ya wananchi.

Simba ambaye pia ni Mratibu wa kampeni wa chama hicho Moshi Mjini, amewataka wananchi kuendelea kudumisha mshikamano na amani katika kipindi cha kampeni na kuhakikisha Oktoba 29, 2025 wote wanaenda kupiga kura na kuichagua CCM.

“Ndugu zangu kura ni tatu kwa CCM, urais tumpe mama yetu Samia Suluhu Hassan, ubunge Ibrahim Shayo na madiwani wote wa CCM katika kata zote 21, tusifanye makosa Oktoba 29,” amesema Simba.