Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbinu kuendeleza biashara za familia hii hapa

Shemane Amin, Mshirika wa ALN Tanzania (kulia), akiendesha mazungumzo na Vineet Verma, Meneja Mkuu wa Kioo Limited, wakati wa hitimisho la mfululizo wa Uendeshaji kimfumo wa biashara za kifamilia ( Family Business Resilience & Growth Knowledge Series), ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya ALN na International Finance Corporation (IFC) jijini Dar es Salaam wiki hii.

Muktasari:

  • ALN Tanzania yasisitiza mifumo ya biashara za familia ili iweze kuendelea vizazi na kupanuka zaidi

Dar es Salaam. Familia zimetakiwa kutumia kutumia mifumo rasmi ya uendeshaji biashara ya utawala bora ili kuhakikisha zinaendelea kudumu vizazi na vizazi na kuvutia uwekezaji kutoka nje.

Hayo yamesemwa huku kukushuhudia baadhi ya biashara za familia zikiporomoka pale mmiliki anapofariki dunia na kutokuwapo kwa msimamizi madhubuti wa kuiendeleza.

Wito huo ulitolewa wakati wa hitimisho la mfululizo wa semina za Family Business Resilience & Growth Knowledge Series, zilizoandaliwa na ALN Tanzania kwa ushirikiano na International Finance Corporation (IFC) jijini Dar es Salaam wiki hii.

Mfululizo wa semina hizo tatu ulijadili misingi ya utawala wa kifamilia, muundo wa bodi na katiba za familia katika awamu zilizopita, huku kikao cha mwisho kikijikita urithishaji na mpito wa uongozi.

Akizungumza katika semina hiyo, Shemane Amin, Mshirika wa ALN nchini, amesisitiza mwendelezo wa biashara za kifamilia hauji kwa mazoea bali unapaswa kupangwa kwa makusudi.

“Biashara nyingi za kifamilia hukua kwa mafanikio katika miaka ya mwanzo kwa kutegemea imani na uamuzi usiyo rasmi,” amesema.

“Hata hivyo, kadri biashara zinavyopanuka na vizazi vinavyoongezeka kushiriki, kuweka mifumo rasmi kunakuwa muhimu kulinda biashara yenyewe na umoja wa familia.”

Amesema kampuni hiyo ilianzisha mfululizo huo wa semina ili kuwapatia wamiliki wa biashara za kifamilia mifumo ya vitendo kuhusu utawala bora, upangaji wa urithishaji na uwazi wa uongozi mambo ambayo mara nyingi huamua iwapo biashara itaendelea baada ya kizazi cha mwanzilishi wa biashara katika familia husika kutoweka.

Edward Williams, Mkurugenzi wa ALN Tanzania, akizungumza wakati wa hitimisho la mfululizo wa kongamano la mafunzo ya uendeshaji kimfumo wa biashara za kifamilia (Family Business Resilience & Growth Knowledge Series), ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya ALN na International Finance Corporation (IFC) jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Edward Williams, Mkurugenzi wa ALN Tanzania, amesisitiza umuhimu wa kuanza mapema kupanga urithishaji na kuonya dhidi ya mabadiliko ya uongozi yanayofanyika kwa dharura.

“Moja ya dhana potofu iliyoenea katika biashara za kifamilia ni kwamba urithishaji huanza pale mwanzilishi anapokuwa tayari kustaafu,” alisema.

 “Kwa uhalisia, urithishaji huanza mapema zaidi. Mabadiliko yenye mafanikio ni yale ambayo ukuzaji wa uongozi, miundo ya wanahisa na mifumo ya utawala inakuwa tayari imewekwa tangu awali,” amesema.

Amesema kadri biashara za Kitanzania zinavyokua kwa thamani na kuwa tata zaidi, mikataba rasmi ya wanahisa, katiba za familia, majukumu yaliyoainishwa wazi kwa watendaji wakuu na mifumo huru ya usimamizi vinakuwa muhimu katika kulinda thamani ya muda mrefu.

Mona Doshi, Mshirika wa ALN kutoka Mombasa nchini Kenya, alizungumzia umuhimu wa sera rasmi za ajira kwa wanafamilia katika kuimarisha uimara wa biashara.

“Kadri familia zinavyopanuka kizazi hadi kizazi, kuwa na mwongozo wa uwazi kuhusu vigezo vya kuajiriwa, viwango vya utendaji na uwajibikaji husaidia kuzuia migogoro ya ndani na kuimarisha uongozi unaozingatia sifa,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya IFC, Rose Lumumba amesisitiza utawala bora uliowekwa kwa mifumo rasmi unahusishwa moja kwa moja na utayari wa kupokea uwekezaji na ustawi wa muda mrefu.

“Biashara za kifamilia zinazoweka mifumo ya utawala mapema huwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuvutia mitaji, kupanuka kwa uwajibikaji na kustahimili mabadiliko ya vizazi,” amesema.