Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madaktari watoa angalizo kushamiri biashara ya figo

Katika kile kinachonekana kukithiri kwa hali ngumu ya maisha, baadhi ya raia nchini Pakistan wameanza kujiingiza katika biashara ya kuuza figo zao kwa watu wenye mahitaji ya kiungo hicho muhimu mwilini.

Wakati wengine wakiuza figo kwa hiyari yao, kuna madai yaliyokanushwa na mamlaka nchini Pakistan, kuwa kuna mitandao unaojihusisha na biashara hiyo kwa kuwateka watu, kuwatoa figo na kuziuza kwa wenye uhitaji.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya madaktari nchini Pakistan wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo huku Dk Ravji Kumar akienda mbali zaidi na kufananisha kinachoendelea nchini humo na biashara ya kuuza figo nchini Nepal.

Kijiji cha Hokse kilichopo umbali wa kilomita 49.2 kutoka Kathmandu ambao ni mji  mkuu wa Nepal, kimepewa jina la utani la ‘kijiji cha figo’, kutokana na ukubwa wa biashara ya uuzaji wa figo  unaofanywa kwenye eneo hilo.

‘’Asilimia kubwa ya wananchi wa kijiji cha Hokse wameuza figo moja…., hali hii ni kama naiona sasa Pakistan. Wengi wanaotoa figo ni wanaokabiliwa na maisha magumu, wanaona bora kutoa figo waweze kuendesha maisha yao ya kila siku,’’ alisema Dk Ravji.

Katika mkutano huo, madaktari hao walidai mbali na umasikini wa watu, kuna utekaji unaendelea ili watu kutolewa figo bila idhini yao.

‘’Februari mwaka huu Muhammad Rafiq aliripoti kwamba binamu yake anayeishi eneo la Rawalpindi, Pakistan alitekwa na mitandao unaojihusisha na biashara ya figo, alisema Dk Ravji.

Alisema matukio hayo yanaendelea licha ya Pakistan kuweka sheria madhubuti za kudhibiti utoaji wa figo, ikitaka iwe kwa utaratibu maalumu chini ya usimamizi wa madaktari.

‘’Watu wnaaotolewa figo kwa sababu tu ya umasikini lakini upasuaji unafanyika bila utaratibu. Ahadi ni kulipwa lakini wapo ambao hawalipwi chochote,’’

‘’Hata malipo yenyewe ya Dola 1,000 hadi 3,000 ni madogo sana ikilinganishwa na gharama za kuishi na figo moja. Kuna kisa cha polisi kubaini mtoto wa miaka 14 kutolewa figo na alipohojiwa alisema alipozinduka alikuta mtu pembeni yake, aliyehisiwa kuwa ndiye aliyewekewa figo yake,’’ alidai Ravji.