Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Biteko aahidi Uyovu kuwa kitovu cha biashara Bukombe

Muktasari:

  • Ametaja miradi mingine ya maendeleo iliyotekelezwa katika kata hiyo ni pamoja na kujenga barabara za mitaa kwa kiwango cha lami, hospitali, zahanati pamoja na mradi wa maji uliogharimu Sh1.1 bilioni.

Bukombe. Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Doto Biteko amesema serikali imeiwezesha Kata ya Uyovu kimaendeleo, hivyo wananchi hao hawana budi kumpigia kura nyingi za ndiyo mgombea wa urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan ifikapo Oktoba 29, mwaka huu.

Dk Biteko ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 17, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni alioufanya Kata ya Uyovu wilayani Bukombe mkoani Geita.

“Hakuna siku ambayo nilimuomba maendeleo Dk Samia kwa ajili ya watu wa Uyovu na Geita akatunyima, ametupa fedha za ujenzi wa barabara nyingi ikiwemo ya kutoka Ushirombo hadi Katoro, hata juzi tulimuomba barabara ya Geita kwenda Nzela hadi Sengerema kwa kiwango cha lami yote haya atatusaidia huyu ni mama ni msikivu,” amesema Dk Biteko. 

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Samia chini ya CCM, katika Kata ya Uyovu wamefanikiwa kujenga shule za msingi 11 na shule binafsi moja kutoka shule tatu, shule za sekondari saba na shule moja ya kidato cha tano na sita. 

Pia, amesema katika Wilaya ya Bukombe, kuna shule mbili za watoto wenye mahitaji maalum na moja ipo Uyovu na nyingine Ushirombo.

Ametaja miradi mingine ya maendeleo iliyotekelezwa katika kata hiyo ni pamoja na kujenga barabara za mitaa kwa kiwango cha lami, hospitali, zahanati pamoja na mradi wa maji uliogharimu Sh1.1 bilioni.

Kuhusu kuifanya Uyovu kuwa kitovu cha biashara, mgombea ubunge huyo amesema Serikali ya CCM itaongeza msukumo kwa kusogeza miundombinu ya kuiwezesha kata hiyo kuvutia shughuli za biashara kwa wingi.

Pia, amesema CCM itatoa mkopo wa Sh200 bilioni kwa vijana na wanawake ili kuwawezesha wafanyabiashara wakiwamo wa Uyovu.

Pamoja na hayo, Dk Biteko amesema miaka mitano ijayo, Uyovu itakuwa na maendeleo zaidi, hivyo wananchi 35,000 wa Kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi Oktoba 29 na kumchagua mgombea urais wa CCM sambamba na mbunge na madiwani wote watokanao na chama hicho.

“Sasa maendeleo haya hayajatokea kwa bahati mbaya kama kuna mtu anatupenda ni Samia, Uyovu ni jeshi kubwa, mkapige kura nyingi ili tuwe na sababu ya kuwaletea maendeleo,” amesema Dk Biteko.

Naye, Mgombea wa udiwani wa Uyovu, Mathayo Kagoma amesema wananchi wa Uyovu wana ajenda moja ya maendeleo na hivyo, amewaomba wananchi hao kuwaamini na kuwapigia kura wagombea wa CCM.

“Ninyi ni mashahidi kwa miaka kumi ya uongozi wa Biteko hapa Bukombe, tumepiga hatua katika elimu na maeneo mengine. Sasa tunasimama hapa tukiwa na shule za msingi 11 katika kata yetu na nyingine zikiendelea kujengwa ili kusaidia watoto wetu,” amesema Kagoma.

Amesema sababu ya kumchagua tena Dk Biteko ni kwa kuwa wanahitaji kupiga hatua ya maendeleo zaidi katika maeneo mengine ikiwemo ya afya.