Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFC inavyosaidia wakulima kupata mbolea kwa urahisi na kwa bei nafuu

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Samuel Mshote.

“Tunawahakikishia wakulima upatikanaji wa mbolea kwa wakati, stahiki na huduma iliyo bora. Mpaka sasa TFC, imefanikiwa kufikisha mbolea katika mikoa, wilaya na kusambaza mbolea kwa kiwango kikubwa tangu ianze huduma ya kuuza mbolea.”

Hii ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Samuel Mshote akizungumzia namna kampuni hiyo ilivyokuwa mkombozi katika upatikanaji wa uhakika wa mbolea kwa wakulima.

Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) ni taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Kilimo ambayo inahusika kusambaza na kuuza aina zote za pembejeo nchini.

TFC ilianzishwa Julai 6, mwaka 1968 chini ya Sheria ya Makampuni (Companies Ordinance CAP 212), ambayo kwa sasa inafahamika kama sheria ya makampuni ya mwaka 2002 (Companies Act 2002 CAP 212) kwa lengo la kusambaza na kuuza aina zote za pembejeo za kilimo zinazotumika nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Samuel Mshote.

Mshote anasema wanafanya kazi ya kusaidia,kutoa taarifa za kitaalam, zinazohusiana na uzalishaji, ubora na viwango vya mbolea ndani na nje ya nchi.

“Tunashirikiana na tasisisi za utafiti katika kufanya utafiti juu ya mbolea na pembejeo nyingine za kilimo hapa nchini. Lengo la kutekeleza majukumu hayo ni kutekeleza azma ya Serikali ya kuwawezesha wakulima kupata pembejeo za kilimo hasa mbolea, kuboresha shughuli zao za kilimo kuwa na tija zaidi, kuzalisha chakula cha kutosha ndani na nje ya nchi,”anasema Mshote.

Anasema majukumu mengine wanayoyatekeleza ni kusaidia wakulima kuona kwa vitendo tofauti ya matumizi sahihi ya mbolea dhidi ya matumizi yasiyofaa, na kwa jinsi ambavyo inahitajika, kuondoa kero ya uelewa mdogo kwa wakulima wadogo, kuwawezesha uelewa wa matumizi ya mbolea, kwa sababu hawana taarifa muhimu za msingi namna nzuri ya kutumia mbolea.

TFC kwa kushirikiana na mamlaka zingine imekuwa ikitoa elimu kwa wakulima ili kuwawezesha kuwa na uelewa juu ya umuhimu wa kuzingatia afya ya udongo. Mengine ni;

Kuhakikisha wakulima wanapata mbolea za uhakika kwa mwaka mzima ili kusaidia uzalishaji thabiti wa kilimo na uzalishaji wa mwaka mzima, kufanya utafiti na maendeleo kwa wakulima, ili kuendeleza uzalishaji wa mbolea na pembejeo za kilimo.

Kushirikiana na vyama vya ushirika na halmashauri ili kuhakikisha utoaji mzuri wa mbolea kwa wakati. Pia TFC imeendelea kuboresha uhifadhi wa mbolea kwa kukamilisha ukarabati wa maghala yanayowezesha kuhifadhi mbolea kwa kipindi chote cha msimu wa kilimo.

Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Kampuni ya mbolea (TFC), inakuza kikamilifu elimu juu ya matumizi bora ya mbolea ili kutanua zaidi matumizi katika maeneo ambayo hayajahudumiwa.

Juhudi hizi zinalenga kuongeza wastani wa matumizi ya mbolea kutoka kilo 19 kwa hekta hadi kilo 50, kulingana na malengo ya maendeleo ya kilimo ya Umoja wa Afrika.

TFC pia inafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na wa karibu na Wizara ya Kilimo chini ya Waziri Hussein Bashe na mashirika yote yaliyo chini ya wizara hiyo kama Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) nk. Vilevile wanashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mimea na Viatilifu (TPHPA) kuhakikisha mbolea zinzouzwa zinakidhi viwango na ubora unaotakiwa.

“Lengo la kutekeleza majukumu haya ni kutekeleza azma ya Serikali ya kuwawezesha wakulima kupata pembejeo za kilimo hasa mbolea, kuboresha shughuli zao za kilimo kuwa na tija zaidi, kuzalisha chakula cha kutosha ndani na nje ya nchi,”anasema Mshote.

Mbolea ikiwa kwenye ghala la TFC Makambako.

Kuhusu changamoto zinazowakabili wakulima katika upatikanaji na matumizi ya mbolea na suluhisho linalotolewa na TFC, Mshote anasema ili kutatua changamoto hizo, kampuni ya mbolea inakamilisha mpango ukarabati wa maghala.

Aidha, TFC imeweza kununua magari matano ya tani 10 kila moja, ili kuwezesha ufikishwaji wa mbolea kwa urahisi katika maeneo husika ya wakulima.

Kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa mbolea bora kwa mwaka mzima ili kukidhi mahitaji ya wakulima wa Tanzania. TFC inalenga kutoa upatikanaji wa mbolea kwa bei nafuu wakati ikizalisha faida ili kuendeleza shughuli zake.

“Kwa sasa tuna mkakati wa kupanua soko letu la mbolea hadi kufikia asilimia 50 ya mbolea yote inayouzwa nchini kuleta maendeleo pasipo kutegemea bajeti ya Serikali,” anasema Mshote.

Anasema kampuni hiyo pia imeanza mchakato wa kufunga mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuchanganya mbolea (blending facility) itakayofungwa bandarini.

Lengo la kufungwa kwa mitambo hii ni kuhakikisha TFC inachanganya mbolea kulingana na mahitaji ya eneo husika kwa sababu ya afya ya udongo, pia itawawezesha wakulima kupata mbolea katika ujazo tofauti kulingana na mahitaji yao. Hii itasaidia wakulima wadogo ambao hawatolazimika kununua mbolea yenye ujazo mkubwa.


TFC inavyosaidia wakulima wadogo kupata mbolea kwa urahisi na kwa bei nafuu

Mshote anasema TFC inawasaidia wakulima wadogo kupata mbolea kwa urahisi na bei nafuu kupitia njia mbalimbali ikiwemo;

Kupitia mpango wa ruzuku ya mbolea ambapo TFC hushirikiana na Serikali hutoa mbolea kwa wakulima kwa bei iliyopunguzwa ili waweze kumudu, kuanzisha vituo vya usambazaji karibu na wakulima wadogo, ili wasisafiri umbali mrefu kutafuta mbolea kufanya kazi na vyama vya ushirika (AMCOS) na vikundi vya wakulima kurahisisha upatikanaji wa mbolea kwa pamoja na kwa masharti nafuu.

Mtaalamu wa TFC akizungumza na mkulima wa mahindi wilayani Moshi.

Kutoa mafunzo kwa wakulima jinsi ya kutumia mbolea kwa ufanisi ili kuongeza tija bila kutumia kiasi kikubwa na katika baadhi ya maeneo, TFC hushirikiana na taasisi za kifedha kutoa mikopo ya pembejeo au kuruhusu malipo kwa awamu.

Mshote ameishukuru Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Kilimo chini ya Waziri Hussein Bashe kwa kuwezesha kuanza upya baada ya kusimama kwa muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya soko.