Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

OSHA inavyochochea mapinduzi ya kidijitali katika usimamizi wa usalama na afya na kazini

Huduma zikiendelea kutolewa katika Banda la OSHA ambaye ni Mwenyeji wa Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani yanayofanyika Kitaifa Mkoani Singida, Viwanja vya Maadhimisho Mandewa kuanzia Aprili 24 hadi 30, 2025.


Katika miongo ya hivi karibu­ni, dunia imeshuhudia maende­leo makubwa ya teknolojia ya kidijitali yaliyogusa nyanja mbalimbali za maisha, ikiwemo sekta ya ajira.

Mojawapo ya maeneo yanay­ofaidika kwa kiwango kikubwa kutokana na mapinduzi haya ni eneo la afya na usalama mahali pa kazi. Teknolojia ya kidiji­tali imeleta mabadiliko chanya katika namna ambavyo waajiri na wafanyakazi wanakabiliana na changamoto za kiafya na kiusalama katika mazingira yao ya kazi.

Mapinduzi haya pia yamewezesha ukusanyaji na uchambuzi wa data kwa kiwan­go kikubwa. Kwa kutumia Akili Mnemba (AI) na ujifunzaji wa kidijitali, kampuni zinaweza kutabiri maeneo au kazi yenye hatari kubwa ya ajali au magon­jwa ya kazini na hivyo kuchukua hatua stahiki za kinga mapema.

Wakati Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, ujumbe wa maadhimisho hayo mwaka huu unasisitiza jambo hili, ukieleza kuwa afya na usalama mahali pa kazi sio wajibu bali ni haki ya binad­amu.

Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani huad­himishwa Aprili 28 kila mwaka kwa lengo la kutafakari, kuweka mikakati na kuboresha juhudi za kitaifa na kimataifa katika kuhakikisha uwepo wa mazin­gira salama ya kufanyia kazi.

Kaulimbiu ya mwaka huu inasema: “Nafasi ya Akili Mne­mba na Teknolojia za Kidijitali katika Kuimarisha Usalama na Afya Mahali pa Kazi”. Kaulimbiu hii inazielekeza nchi kutumia mifumo na njia za kidijitali kati­ka kuhakikisha usalama na afya kazini unaeleweka, unafuatwa na kuboreshwa.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Hadija Mwenda.



Kwa Tanzania, mapinduzi haya yameanza kuonekano kwa vitendo kupitia kazi kub­wa inayofanywa na Mamlaka ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) hususan katika kubuni na kutumia mifumo ya kidijitali katika kusimamia usalama na afya kazini.

Ikiwa na zaidi ya miongo miwili toka kuanzishwa kwake, OSHA imejiapambanua kama nguzo muhimu katika kusi­mamia masuala ya afya na usal­ama mahali pa kazi nchini kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa mazingira ya kazi salama na wafanyakazi wenye afya njema katika sekta zote.

Tangu kuanzishwa kwake, OSHA imejidhatiti kuhakiki­sha kwamba usalama haupo tu kwenye makaratasi au matan­gazo ya ukutani, bali ni kitu ambacho kinatakiwa kupewa kipaumbele katika shughuli za kila siku.

Mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 pekee, OSHA ili­fanya kaguzi za jumla (general inspections) 23,712 na kaguzi maalum (specific inspections) 331,874 na kutoa miongozo ya utekelezaji wa kitaalam. Kaguzi hizi zimesababisha maboresho katika utayari wa kukabiliana na majanga ya moto, utunzaji wa kemikali, miitikio ya dharu­ra na utumiaji wa vifaa vya kujikinga (PPE).


Matumizi ya mifumo ya kidi­jitali

OSHA ni miongoni mwa Taa­sisi za Umma ambazo zinaon­goza katika matumizi ya mifu­mo ya kidijitali jambo ambalo limesaidia kuleta mapinduzi makubwa kwenye masuala ya usalama na afya kwenye mae­neo ya kazi.

Sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu, OSHA imeanza kutumia mifumo ya kidijitali ili kuboresha jinsi inavyotekeleza majukumu yake muda mrefu. Mamlaka hiyo imebuni mifumo ya ukaguzi ya kielektroniki, usajili wa kidijitali na majuk­waa ya mafunzo ya mtandaoni ambayo yanarahisisha waajiri na wafanyakazi kupata nyenzo muhimu za usalama.

Mifumo hii inaboresha ufani­si, uwazi na ufikiaji. Waajiri sasa wanaweza kusajili mae­neo yao ya kazi, kuwasilisha nyaraka za kisheria kwa njia ya mtandao, kupokea ripoti za ukaguzi kidijitali na kushiriki katika mafunzo bila kuhitaji kusafiri hadi ofisi za OSHA. Hii pia imeleta manufaa makubwa kwa wafanyakazi walio katika maeneo ya mbali au ambayo hayajafikiwa na huduma hizo.

Sehemu ya mwanzo ya mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Maeneo ya Kazi.

OSHA pia inaangalia uweze­kano wa kuanza matumizi ya Akili Mnemba (AI) ambayo yanaweza kusaidia kutambua vihatarishi mahali pa kazi kwa usahihi zaidi na kwa wakati sahihi. Kupitia programu za majaribio, mamlaka hiyo inajaribu kuona ni jinsi gani uchanganuzi wa data unaweza kutabiri ukiukwaji wa sheria za usalama na afya kabla hauja­tokea na kuweza kuuzuia bada­la ya kusubiri utokee.

Mabadiliko haya hayana len­go la kuondoa kabisa matumizi ya rasilimali watu, bali kuimari­sha mifumo ya usalama na afya na kuifanya kuwa bora na sahi­hi zaidi ili kuweza kukabiliana na changamoto za mazingira ya kazi.


Utoaji wa mafunzo ya usalama na afya kazini

Mafunzo ni nguzo ya utekelezaji wa shughuli za OSHA. Mwaka uliopita, zaidi ya wafanyakazi 21,462 na maafisa wa usalama na afya walipatiwa mafunzo kupitia programu zilizoidhinishwa na OSHA. Mafunzo haya yalihusi­sha kila kitu kuanzia utambuzi wa hatari na njia za kuepuka au kukabiliana na hatari husika pamoja na matumizi sahihi ya mashine na kemikali.

Kampeni za uhamasishaji kwa umma pia zimeongezeka kwa kiasi kikubwa, huku OSHA ikitumia redio, televisheni, mitandao ya kijamii na ush­iriki wa jamii kueneza ujumbe muhimu. Kampeni hizi zinalen­ga waajiri na wafanyakazi na kufanya afya na usalama kuwa dhamira ya pamoja.


OSHA na mkakati wa kufikia sekta isiyo rasmi

Licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ras­mi, sekta isiyo rasmi, ambayo inahusisha zaidi ya asilimia 80 ya nguvu kazi ya Tanzania, bado inakabiliwa na changa­moto kubwa za kiusalama.

Wafanyakazi katika sekta hii mara nyingi hufanya kazi bila mikataba rasmi, zana za usala­ma au mafunzo. Hawa ni pamo­ja na waendesha bodaboda, wachimbaji wadogo, wafanya biashara ndogo ndogo masoko­ni, wafanyakazi wa majumbani na wauzaji wa chakula mitaani (mama na baba lishe).

Ili kukabiliana na hili, OSHA imeanzisha programu za kufikia jamii kupitia utoaji wa taarifa za usalama na afya kwa lugha ya Kiswahili hususani kupitia program maalum ya mafunzo ijulikanayo Afya Yan­gu-Mtaji Wangu inayoyalenga makundi mbalimbali ya waja­siriamali wadogo. Kwa kutu­mia njia hii, OSHA imewezesha ufikishaji wa taarifa za afya na usalama kazini kuwa rahisi na hivyo kuwafanya watu kuchu­kua hatua za kujilinda wenyewe na kuwalinda wengine.

OSHA ina mkakati wa kuunganisha wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi kwe­nye mifumo yake ya usajili na usaidizi wa kidijitali ili kurahi­sisha wafanyabiashara wadogo katika sekta isiyo rasmi kupata mafunzo na kuzingatia mahi­taji ya kimsingi ya usalama bila kuwepo kwa urasimu wa aina yoyote.


Usalama kama uwekezaji wa kimkakati

Leo hii, kufuata kanuni za OSHA hakuonekani tena kuwa suala gumu ama lenye urasimu, bali umekuwa uamuzi muhimu na wa kimkakati katika biasha­ra. Kampuni za Tanzania amba­zo zimeweka kipaumbele kati­ka masuala ya afya na usalama zinashuhudia kupungua kwa matukio ya ajali mahali pa kazi, huku zikiinua ari za wafanyaka­zi wake na utendaji bora kwa ujumla.

Katika sekta zenye hatari kubwa kama vile ujenzi, uchu­kuzi na uzalishaji, kampuni kadhaa zimepunguza ajali zin­azotokea mahali pa kazi kwa kiwango kikubwa baada ya kufuata kanuni za OSHA. Hii inathibitisha kuwa usalama sio gharama, ni uwekezaji kwa watu na tija katika uzalishaji.

Kampuni nyingi sasa zina­jumuisha masuala ya usalama na afya katika mipango yao ya utendaji kazi, sio tu ili kufikia viwango vya kisheria, lakini kuvutia vipaji na ubunifu, kuon­geza mauzo na kushindana katika masoko ya kimataifa.


Utekelezaji wa Matamko na Mikataba ya Kimataifa

OSHA inatekeleza kwa viten­do matakwa ya Mikataba na Matamko ya Kimataifa kama vile Mkataba wa ILO Na. 155 wa Usalama na Afya Kazini, pamo­ja na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), hasa Lengo la 8 kuhusu za Kazi Zenye Stahaha na Uku­aji wa Uchumi.

Kwa msaada wa washirika wa kimaendeleo, OSHA imewekeza katika tafiti na uvumbuzi ili kukabiliana na changamoto zitokanazo na shughuli. Kadiri uchumi wa Tanzania unavyo­endelea kuwa wa kisasa, OSHA imedhamiria kuhakikisha kuwa teknolojia inaboresha utu wa binadamu na si kuhatarisha.

Maendeleo ya Tanzania kati­ka usalama na afya mahali pa kazi yanaridhisha, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Sekta isiyo rasmi lazima iju­muishwe kikamilifu, elimu ya usalama lazima itolewe kuan­zia shuleni mpaka vyuoni.