Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa EACOP LTD na WASCO ISOAF watoa ufadhili wa masomo kwa vijana wa Kitanzania 124

Kupitia Mpango wa Ufadhili wa Masomo wa EACOP na WASCO ISOAF, jumla ya wanafunzi 124 wa Kitanzania wamepata ufadhili  wa masomo, ikiwa ni ushahidi thabiti wa kujitolea kwa kampuni hizo katika maendeleo ya jamii. Hafla ya uzinduzi iliyofanyika chuo cha VETA Tabora ni hatua muhimu katika juhudi za kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi kwa ajili ya sekta ya nishati inayokua nchini Tanzania.

Viongozi wa kijamii, wawakilishi kutoka EWURA, TPDC, VETA, pamoja na maafisa waandamizi wa serikali walihudhuria hafla hiyo. Akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi wa Mradi wa WASCO ISOAF, Gary Deason alisema, "Leo tunawekeza katika mustakabali wa baadae, hatutoi tu ufadhili wa masomo." Aliongeza kuwa mpango huu utaimarisha familia, kuboresha maisha, na kuweka msingi wa maendeleo ya baadaye ya taifa.

Kwa kuongezwa kwa idadi hii ya wanafunzi waliopata ufadhili wakimasomo, EACOP sasa imefadhili jumla ya wanafunzi 216. Mpango huu ni sehemu ya mkakati mpana wa kutoa elimu ya kiufundi yenye ubora wa hali ya juu, kwa kushirikiana na taasisi kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Ufundi Arusha, na vituo mbalimbali vya VETA.

Zaidi ya vijana wa kitatanzania 71 wamepata nafasi za mafunzo kwa vitendo ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na China, Afrika Kusini, Umoja wa Falme za Kiarabu, na Ufaransa, kama sehemu ya juhudi za maudhui ya ndani za EACOP. Ili kuboresha ubora wa ufundishaji wa kiufundi nchini kote, programu ya kufundisha wakufunzi (Train-the-Trainer) imewafundisha walimu zaidi ya 250.

"Tunajivunia kuunga mkono mpango huu wenye faida kubwa na tumejizatiti kutoa mafunzo bora kwa hawa wanufaika," alisema Dkt. Zebedayo Kyomo, Mkuu wa VETA Tabora.

Zaidi ya kampuni ndogo na za kati (SMEs) 100 nchini Tanzania zimepatiwa mafunzo kupitia Mpango wa kuongeza ujuzi kwa taasisi ndogo na za kati (Industrial Enhancement Centre) kuhusu teknolojia za kisasa za mabomba na kanuni za usalama, jambo ambalo limeongeza ushiriki wao katika mnyororo wa thamani wa mafuta na gesi. Katika kilele cha utekelezaji wa mradi, zaidi ya watanzania 6,763 wataajiriwa, huku zaidi ya masaa milioni ishirini nan ne (24) ya kazi yakitolewa na wafanyakazi, na zaidi ya masaa laki tatu arobaini na saba (347,000) yakitumika kuwapa mafunzo wafanyakazi wa ndani.

"Hii ni uwekezaji wa muda mrefu kwa vijana ambao watakuwa wahandisi na wavumbuzi wa baadaye wa Tanzania," alisisitiza Geofrey Mponda, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa EACOP. Neema Kweka, Meneja wa Maudhui ya Ndani wa EACOP aliongeza, "Safari ya EACOP inaonesha dhamira ya watu, utendaji na ustawi. Hatujengi tu bomba, tunajenga urithi wa kweli."

Mkuu wa Wilaya ya Nzega aliipongeza hatua hii kuwa ni mfano wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, na kuitaja kama hatua muhimu ya kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii.

Mbali na kusherehekea fursa ya elimu, hafla hii ilisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuijenga Tanzania yenye maarifa na mafanikio endelevu.