Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka minne ya uongozi wa Rais Dk Samia: UDSM yatathmini mafanikio yake

Moja kati ya majengo 24 yanayojengwa na UDSM kupitia mradi wa HEET. Jengo hili liko katika Taasisi ya Sayansi za Bahari ya UDSM, Buyu Zanzibar. Majengo mengine yanajengwa Dar es Salaam, Kagera na Lindi.

Kwa kipindi cha miaka minne tangu aingie madarakani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk Samia Suluhu Hassan, amedhihirisha uongozi thabiti, mahiri na wenye maono. Chini ya uongozi wake, Tanzania imepiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali, ikiwemo elimu ya juu, miundombinu, sekta ya viwanda, maendeleo ya nishati na usimamizi bora wa rasilimali za umma.

Ni kwa muktadha huu, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mheshimiwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete, Baraza la Chuo, Menejimenti na jumuiya nzima ya UDSM wanatoa pongezi za dhati kwa Dk Samia kwa mafanikio haya.


Miradi ya kimkakati UDSM

Katika kipindi hiki cha miaka minne, UDSM kimeweza kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo imekuwa nguzo muhimu katika kutimiza malengo na majukumu makuu yake yaani kutoa maarifa, kufanya tafiti na ubunifu na kutoa huduma kwa jamii.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Balozi Mwanaidi Maajar (kulia) wakiwa kwenye moja ya mahafali ya UDSM.




Mradi wa HEET

Ndani ya miaka minne kuan¬zia mwaka 2021, chuo kinaendelea kutekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia utakaokamilika mwaka 2026, ambapo UDSM kimetengewa Dola za Marekani milioni 49.5, ambazo zimejikita katika ujenzi wa majengo mapya 24, ikiwa ni pamoja na maabara, ubore¬shaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, malazi ya wana-funzi na vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia kama vile madarasa janja na vifaa vya kisasa vya maabara.

Mradi huu wa HEET si tu umechangia katika miundom¬binu bali pia katika kubadili mita¬ala kuwa ya kimkakati na yenye kupelekea kuzalisha wahitimu wanaoshindana katika soko ya ajira kimataifa. Mradi pia ume-somesha wanataaluma 22 kwa masomo ya Uzamivu 12 na Uma¬hiri 10 katika vyuo bora kimatai¬fa.

Kupitia mradi huu, Rais Samia amewezesha kuongezwa kwa kampasi na vyuo vikuu vingine katika maeneo mengi nchini ili kuwezzesha upatikanaji wa elimu ya juu kwa Watanzania wengi zaidi.

Mradi huu umefanikisha kuboresha mashirikiano kati ya taaluma na sekta za uzalishaji (academic-industry linkage) kwa kushirikisha wanatasnia amba¬po wanataaluma wanajifunza kwa vitendo yale wanayoyapata kwenye vitabu, nadharia na tafiti ili kuongeza maarifa na uthabiti katika ufundishaji.

Muonekano wa mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Shule Kuu ya Uchumi.

Katika kipindi cha 2021-2025, UDSM imefanya mapitio ya mita¬ala zaidi ya 120 katika ngazi ya shahada za awali na uzamili. Len¬go kuu limekuwa ni kuhuisha na kuoanisha kozi na ujuzi unaohi¬tajika katika soko la ajira, sam¬bamba na mwelekeo wa kisera wa kitaifa kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023.

Baadhi ya maboresho yaliyo¬fanyika ni pamoja na kuingiza masomo ya uendelevu wa mazin¬gira, ujasiriamali, sayansi ya data, akili mnemba (AI) na maa¬dili ya kazi katika mitaala yote ya shahada ya kwanza; kuongeza mafunzo ya vitendo kupitia mira¬di ya wanafunzi, mafunzo kazini (industrial/practical training) na vituo vya ubunifu (innovation hubs); na kuweka mfumo wa mta¬ala shirikishi wa vyuo vikuu na sekta za uzalishaji (Industry-Ac¬ademia Curricular Alignment).


Mradi wa kuongeza ghorofa mbi¬li Bloku ‘A’ na ‘E’, Hosteli ya Dk Magufuli

UDSM katika kukabiliana na upungufu wa mabweni ya wana¬funzi katika kampasi ya Mwalimu J.K Nyerere, Mlimani kikiwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 11,115 ikilinganishwa na wana¬funzi 22,000 wanaohitaji malazi, kimetekeleza mradi wa kuongeza ghorofa mbili kwenye Bloku A na E katika hosteli ya Dk Magufuli.

Mradi huu unatekelezwa kupi¬tia fedha zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolo¬jia (WyEST) kufuatia maombi ya chuo. Kwa ujumla, hosteli hii ina jumla ya bloku sita (Bloku A, B, C, D, E na F) zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 Kwa awamu ya kwanza, nyongeza ya ghorofa mbili imefanyika katika bloku mbili (A na E) kwa kipindi cha mwaka 2022 hadi 2024.

Kwa gharama ya Sh 3,873,482,450 mradi huu umewezesha nyongeza ya gho¬rofa katika Bloku A na E ambapo utekelezaji ulianza Novemba 28, 2022, ulikamilika Mei 5, 2024.

Nyongeza hii imesaidia wana¬funzi 576 (wanawake 192, na wanaume 384) kupata malazi kwenye hosteli hizo. Kwa ujum¬la kukamilika kwa hosteli zote kutaongeza idadi ya wanafunzi hadi kufikia 4,416 kutoka 3,840 wa sasa. Ongezeko hili litasaidia kupunguza uhaba wa mae¬neo ya malazi kwa wanafun¬zi na pia kuboresha mazin¬gira ya kujifunzia.


Ujenzi wa kituo cha wana¬funzi katika Kampasi ya Mwl. J.K. Nyerere

Katika kipindi hiki UDSM imeendelea kutekeleza Mra¬di wa Kituo cha wanafunzi unaohusisha ujenzi wa jen¬go lenye jumla ya ghorofa nne za juu na ghorofa mbili za chini.

Mradi huu unakusudia kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia kwa wanafunzi. Aidha kituo hiki kitakuwa na maeneo kwa ajili ya ofisi, vyakula na vinywaji huduma za kifedha maduka, steshenari na mga-hawa/Kafeteria. Pia kutaku¬wa na kumbi za mikutano na ukumbi wa mazoezi.


Ujenzi wa jengo la Shule Kuu ya Uchumi

Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Shule Kuu ya Uchu¬mi uliendelea kupitia fedha za Serikali Sh 9,783,180,213. Mradi huu unahusisha ujen¬zi wa majengo kwa ajili ya ofisi, madarasa, vyumba vya semina, vyumba vya kompyuta, jengo la mihad¬hara, maegesho ya magari na mengine. Kukamilika kwa jengo hili kutakuwa chachu ya kuongeza udahili wa wanafunzi UDSM, kukuza utafiti wa masuala ya taalu¬ma ya uchumi na kusaidia katika maamuzi mbalimbali kisera. Mradi huu unataraji¬wa kukamilka tarehe 30 Mei 2025.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dk Doto Biteko (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu alipofanya ziara katika kituo mama cha kujaza gesi asilia kwenye magari

Ujenzi wa kituo mama kwa ajili ya kujaza gesi asilia kwenye magari na karaka¬na ya kubadilisha mifumo ya magari ili kutumia gesi asilia

Chuo kinatekeleza mradi huu na mkandarasi Sinoma East Africa Co., Ltd kwa ush¬irikiano na Sinoma Interna¬tional Engineering Co. Ltd huku gharama za ujenzi pamoja na usimamizi ukiwa chini ya Shirika la Maende¬leo ya Petroli Tanzania (TPDC). Mradi ulianza Mei 23, 2024 na hivi karibuni utakamilika na kuzinduliwa rasmi.

Mradi huu utakaohusisha kituo mama chenye eneo la kujazia gesi asilia kwenye vyombo vya moto pamoja na karakana itakayotumika kubadili mifumo ya magari na vyombo vingine vya usafiri kutoka matumizi ya mafuta kwenda matumizi ya gesi asilia unatekelezwa kwa makubaliano maalum kati ya UDSM na TPDC. Kituo hiki pia kitatumika kama eneo la mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa UDSM ili kupata elimu na ujuzi unaoendana na maba¬diliko ya teknolojia.


Mageuzi ya mitaala kwa kuendana na mahitaji ya soko la ajira

Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimefan¬ya mageuzi ya kimkakati ya mitaala yake ili kuendana na mabadiliko ya kijamii, kisay¬ansi, na kiuchumi, sambam¬ba na mahitaji halisi ya soko la ajira kitaifa na kimataifa.

Zaidi ya mitaala 120 katika ngazi ya shahada ya kwanza na uzamili imefany¬iwa mapitio na maboresho makubwa kwa kuzingatia, mwelekeo wa elimu inayo¬tegemea ujuzi (competen¬cy-based education); uju¬muishaji teknolojia mpya kama akili mnemba (AI), sayansi ya data, ujasiriama¬li, maadili ya kazi, na uen¬delevu wa mazingira; ush¬irikishwaji wa wadau kutoka sekta binafsi na tasnia (aca¬demic-industry linkage); kuimarisha mafunzo kwa vitendo kwa kutumia mira¬di ya wanafunzi, vituo vya ubunifu (innovation hubs), na mafunzo kazini (industri¬al training).

Mageuzi haya yame¬fanyika sambamba na mwelekeo wa kisera wa kitaifa kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023, kuzingatia miongo¬zo ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), hususan Mfumo wa Uandaaji wa Mitaala (2021) na Mfumo wa Sifa za Chuo Kikuu (UQF), na yamejumuisha masuala mtambuka kama usawa wa kijinsia, matumizi ya TEHA¬MA, mabadiliko ya tabi¬anchi, mikakati mahususi ya Maendeleo ya Taifa; na mwelekeo wa karne ya 21.

Hatua hii ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya Serikali ya awamu ya sita ya kuhaki¬kisha elimu ya juu nchini inakuwa kichocheo kikuu cha mageuzi ya uchumi wa Taifa.


Ongezeko la udahili kwa ngazi zote za masomo

Katika kipindi cha 2021/2022 hadi 2024/2025, idadi ya wanafunzi walioda¬hiliwa UDSM imeongezeka kutoka 15,408 hadi 16,956, sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 10. Hili limechangi¬wa kwa kiasi kikubwa na jiti¬hada za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuongeza uwezo wa chuo katika rasilimali watu wa miundombinu. Hii imesababisha kuimarika kwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Pia kume¬saidia ongezeko la idadi ya wanafunzi UDSM. Kuan¬zishwa kwa Samia Schol¬arship Fund mwaka 2022, inayolenga kuwawezesha wanafunzi wa kada za say¬ansi, tiba, na uhandisi.


Uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya kujifunzia

Serikali chini ya uongozi madhubuti wa Mheshimiwa Rais Dk Samia, imewekeza kwa kiwango kikubwa kati¬ka kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia ikiwemo maabara za kisasa, madarasa, maktaba na vifaa vya kufundishia.

Mathalani kupitia mradi wa HEET, UDSM imenufaika kwa kiasi cha USD milioni 49.5, kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya 24, yakiwe¬mo madarasa ya kisasa, hos¬teli, maabara za kisasa, na vituo vya mafunzo kupitia kidijiti (e-learning), ununuzi na usimikaji wa ubao shirik¬ishi (interactive smart boards), mifumo ya kusaid¬ia kusikiliza mihadhara (lec-ture capture systems), vifaa vya kidijiti vya kushirikisha (digital collaboration tools), majukwaa ya akili unde (AI-driven platforms), na suluhisho za kisasa za uwepo (telepresence).

Mwonekano wa jinsi litakavyokuwa jengo la kituo cha wanafunzi katika Kampasi ya Mwl. J.K. Nyerere litakapokamilika.

Pia kumekuwa na ubore¬shaji mkubwa wa maktaba kuu, ikiwemo kuanzishwa kwa sehemu ya utunzaji wa kidijiti (Digital Repository) na kupanua upatikanaji wa vitabu vya kusoma kidiji¬ti (e-books), usimikaji wa vifaa vya kisasa vya mul¬timedia kwa ajili ya kumbi za mihadhara kama vile projekta za Android zenye uwezo mkubwa, majukwaa ya dijiti, na mifumo ya hali ya juu ya sauti.

Uwekezaji huu umeonge¬za sana ubora wa mazingira ya kujifunzia, kuimarisha upatikanaji wa maarifa, na kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu ya juu kwa njia ya kidijitali.

Uanzishaji wa programu mpya za masomo zenye mvuto wa kimataifa

Katika kukidhi mahitaji ya mabadiliko ya teknolo¬jia, mazingira ya kiuchumi na kisera na kwa kutambua mabadiliko ya kijamii, kisay¬ansi na kiuchumi, UDSM imeanzisha programu mpya za shahada na uzamili katika maeneo ya kimkakati kama vile Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Sayan¬si ya Data, Nishati Jadidi¬fu, Biashara ya Kimataifa, Usimamizi wa Mazingi¬ra, sheria za kimataifa, na uhandisi wa kisasa. Pro¬gramu hizi zimeundwa kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi na mashirika ya kimataifa ili kuhakikisha kuwa wahitimu wanakuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira la sasa na la baadaye.

Baadhi ya programu hizo ni: Shahada ya Awali ya Say¬ansi katika Akili Mnemba na Ujifunzaji wa Mashine (BSc in Artificial Intelligence and Machine Learning) inayo¬tolewa na Ndaki ya TEHA¬MA (CoICT); Shahada ya Umahiri ya Sayansi katika Teknolojia za Nishati Jadid¬ifu (MSc in Renewable Ener¬gy Technologies) inayotole¬wa na Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET); Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Jinsia, Maendeleo na Uju¬muishwaji wa Kidijitali (MA in Gender, Development and Digital Inclusion) inayotole¬wa na Taasisi ya Masomo ya Maendeleo (IDS), Sha¬hada ya Awali ya Biashara katika Masoko ya Kidijitali na Uchanganuzi (BCom in Digital Marketing and Ana¬lytics) inayotolewa na Shule Kuu ya Masomo ya Biashara (UDBS) na Shahada ya Uma¬hiri ya Uchumi wa Buluu na Sera za Baharini (MSc in Blue Economy and Marine Policy) inayotolewa na Taa¬sisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar.

Programu hizi zinacho¬chea maarifa na stadi zin¬azohitajika katika uchumi wa kisasa, na ni ushahidi wa uwezo wa UDSM na Seri¬kali katika kutafsiri dira ya maendeleo ya Taifa kupitia elimu bora na bunifu.


Tafiti muhimu zilizofanyika

Katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Has¬san, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimefanya tafiti na ubunifu mbalimba¬li katika nyanja tofauti kwa lengo la kuchangia maende¬leo ya Taifa. Tafiti na mira¬di hii inaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo, kila moja likiwa na mifano na vyanzo vya taarifa husika:


Utafiti na Ubunifu kwa Manufaa ya Jamii Tanzania

Katika kundi hili ipo mifa¬no kadhaa ya tafiti amba¬zo zimefanyika na watafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama vile Mfumo Jumuishi wa Taarifa kwa Uwezeshaji wa Watoto wa Mitaani katika Mazingira yenye Rasilimali Chache Tanzania. Mradi huu unalen¬ga kuunda mfumo wa kidiji¬tali utakaosaidia watoto wa mitaani kwa kuwatambua, kuwahifadhi kwenye kanzi¬data, na kuwaunganisha na huduma za jamii kama elimu na afya. Lengo ni kuwasaid¬ia watoto wa mitaani kati¬ka maeneo yenye rasilimali finyu.

Upo pia mradi wa iCare¬Connect+ ambao ni Maaba¬ra ya DHIS2 ya UDSM. Kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, UDSM ilitengeneza mfumo wa wavuti kwa ajili ya vituo vya afya kufuatilia safari za wagonjwa. Mfu-mo huu umeanza kutumika katika Hospitali ya UDSM na unalenga kuboresha usima¬mizi wa taarifa za wagonjwa na huduma za afya. Ni mfu¬mo wa kidijitali, uliobuni¬wa na Maabara ya DHIS2 ya UDSM kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, unalen¬ga kuboresha huduma za afya kwa kufuatilia safari ya mgonjwa katika ngazi za zahanati, vituo vya afya, na hospitali. Mfumo huu ume¬boresha utoaji wa huduma za afya kwa kurahisisha upa¬tikanaji wa taarifa za wag¬onjwa na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa taarifa za afya.


Tafiti za Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi wa Kidigitali

Katika kundi hili kuna tafi¬ti kama vile Smart Urban Farming Initiative ambao ni mradi huu unaochanganya matumizi ya sensa za IoT, umwagiliaji wa maji wa moja kwa moja, na udhibiti wa hali ya hewa ili kuwezesha kilimo cha wima katika mae¬neo ya mijini kama Dar es Salaam. Mfumo huu unalen¬ga kuongeza uzalishaji wa chakula kwa kutumia nafasi ndogo na teknolojia rafiki kwa mazingira.

Pia kuna mradi wa mfumo wa Akili Mnemba kwa ajili ya Usimamizi wa mahud¬hurio ya wanafunzi wakati wa Mihadhara na Mitihani. Mradi huu unalenga kubuni mfumo wa kutumia Akili Bandia (AI) na data kutam¬bua na kusimamia mahud¬hurio ya wanafunzi kwenye mihadhara na mitihani, hivyo kuboresha usimamizi wa rasilimali watu katika taasisi za elimu ya juu.

Tafiti za Uchumi wa Buluu na Sayansi Akua (Bahari na Maziwa)

Katika kipindi hiki, Chuo kimetekeleza miradi ya aina hii Suluhisho Bunifu la Uvuvi kwa Uhifadhi na Uendelevu wa Uchumi wa Buluu Tan¬zania: Mradi huu unalenga kubuni teknolojia za kisasa za uvuvi ili kuongeza mavu¬no na kupunguza hatari kwa wavuvi, hivyo kulinda rasilimali za maji na kukuza uchumi wa buluu nchini.


Tafiti za Maendeleo ya Kijamii, Siasa na Uchumi

Katika kundi hili, Chuo kimetekeleza tafiti kama vile Uandishi wa Wasifu wa Julius Nyerere. Hiki ni Kitabu chenye juzuu tatu kiitwacho “Development as Rebellion: Julius Nyerere, a Biography” kimeandikwa na maprofesa wa UDSM, kikitoa mwanga juu ya mai¬sha, mawazo, na mchango wa Nyerere katika siasa na maendeleo ya Tanzania.

Mradi mwingine ni ule wa Ushirikiano wa UNESCO CFIT III na UDSM ambao unalenga kuongeza uwezo wa vyuo vikuu kujibu mahi¬taji ya ujuzi kwa maende¬leo ya Taifa kwa kuwezesha ushirikiano kati ya vyuo vikuu na sekta za uzalisha¬ji, kuboresha ufundishaji unaoendana na soko la aji¬ra na kuimarisha ujifunzaji unaozingatia umahiri. Pia kuna mradi wa Youth for Children (Y4C) Innovation Hub.

Hiki ni Kituo kilichoan¬zishwa kwa ushirikiano kati ya UDSM na UNICEF Tanzania, kinatoa mafun¬zo na rasilimali kwa vija¬na ili kubuni suluhisho za kibunifu zinazochangia katika kufanikisha malen¬go ya maendeleo endelevu. Kupitia kituo hiki, miradi mbalimbali imeanzishwa na vijana kwa lengo la kutatua changamoto za kijamii.


Serikali inavyonufaika na tafiti na ubunifu kutoka UDSM

Serikali ya Tanzania inan¬ufaika kwa njia mbalimbali kutokana na tafiti na ubuni¬fu unaofanywa na UDSM. Manufaa haya yapo katika aina anuai kama vile Ubore¬shaji wa Huduma za Jamii ambapo Tafiti za UDSM hutoa suluhisho za kisay¬ansi na kiteknolojia zinazo¬boresha huduma za jamii, kama vile afya, elimu, na miundombinu.

Kupitia tafiti za UDSM, kumekuwa uendelezaji wa sera na mikakati. Matokeo ya tafiti husaidia serikali katika kubuni na kutekeleza sera na mikakati inayolenga maendeleo endelevu katika sekta mbalimbali. Tafiti hizi pia zimepelekea ushirikiano katika Miradi ya Maende¬leo. UDSM inashirikiana na Serikali katika miradi ya maendeleo, kama Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadi¬liko ya Kiuchumi (HEET), unaolenga kuboresha miundombinu ya elimu na kuongeza uwezo wa udahili katika programu za uhandi¬si, sayansi, na teknolojia.

UDSM kwa kupitia tafiti zake pia imesaidia uende¬lezaji wa Uchumi wa Kidig¬itali. Tafiti na ubunifu kati¬ka teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka UDSM zinachangia katika kuimar¬isha uchumi wa kidigitali, jambo linalosaidia Serikali katika kuboresha huduma za umma na kuongeza ufani¬si katika utawala.


UDSM inavyohakikisha tafi¬ti zinatatua changamoto za kijamii na kiuchumi

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba matokeo ya tafi¬ti zake yanatumika katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi nchini Tanzania kama vile kuan¬zisha Ajenda ya Utafiti ya UDSM. Ajenda hii inaeleke¬za shughuli za utafiti za chuo katika kushughulikia changamoto kuu za kijamii na kusaidia mchakato wa Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda. Inasisitiza ush¬ irikiano wa taaluma mbalimbali, mbinu madhubuti za ukusanya¬ji data, na maadili ya utafiti ili kuhakikisha matokeo yenye ath¬ari.

UDSM imeandaa pia mwongo¬zo wa Huduma za Jamii na Ush¬irikiano. Mwongozo huu unalen¬ga kushughulikia mahitaji ya kijamii na kiuchumi kwa kukuza matumizi ya matokeo ya utafiti na ubunifu. Mwongozo huu pia unalenga kuendeleza ushirikiano wa kimkakati kati ya chuo na taa¬sisi nyingine, kuwezesha vikun¬di vya jamii vilivyo pembezoni kwa kutoa programu maalum za huduma za jamii.

UDSM pia inashirikiana na wadau wa nje katika kushughu¬likia changamoto za kijamii, kuchangia katika malengo ya maendeleo endelevu, na kutoa suluhisho kwa masuala muhimu katika sekta kama afya, kilimo, nishati, na uhifadhi wa mazin¬gira. Ushirikiano huu unasaidia kutafsiri matokeo ya utafiti kuwa manufaa halisi kwa jamii.


Utoaji wa huduma za ushauri wa kitaalamu

UDSM kina jukumu muhimu la kutoa huduma za ushauri wa kita¬alamu kwa sekta ya umma na bin¬afsi. UDSM ina uwezo mkubwa wa kutoa huduma bora za ushauri wa kitaalamu, kupitia wataala¬mu wake imekuwa ikisaidia sekta mbalimbali za umma na binaf¬si. Huduma hizi zimekuwa ndio chachu ya maendeleo anuai kama vile afya, ujenzi na miundombinu na teknolojia. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimejidhihir¬isha kama kinara wa kitaifa na kikanda katika utoaji wa huduma kwa umma kupitia tafiti zenye tija na kazi za ushauri.

Katika kipindi cha miaka hii minne, Serikali imesaidia kubore¬sha miundombinu na kuwajen¬gea uwezo Wahadhiri na Watafiti katika kufanya tafiti na bunifu mbalimbali. Hii imesaidia watafiti hao kupata fedha nyingi kwa ajili ya huduma za utafiti na ushauri. Pamoja na hayo, wapo wataalamu kutoka UDSM ambao wameshiri¬ka katika kuandaa rasimu ya Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050. Aidha, hivi karibuni wataa¬lamu wengine waliteuliwa kuun¬da kamati ya kuandaa Mpango wa Pili Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Mkumbi II) au Blueprint 2.0.

Mafanikio haya yanaonyesha dhamira ya Serikali kuiweze¬sha UDSM kushughulikia mahi¬taji halisi ya jamii kwa kutumia mbinu za kimkakati zinazotege¬mea ushahidi wa kisayansi.


Ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili

Serikali ya Rais Samia imesaid¬ia UDSM kujikita katika kuku¬zaji wa lugha ya Kiswahili na utamaduni wetu kimataifa. Hii ni pamoja na kuanzisha mpango wa ufadhili kwa wanafunzi wa Afrika wanaotaka kusoma Shahada ya Umahiri ya Kiswahili hapa UDSM. Pia, chuo kimeanzisha programu za kufundisha Kiswahili katika nchi kama Afrika Kusini, Zambia, Ethiopia, Ghana, Sudan Kusini, Namibia, na Cuba. Mfano mzuri ni uzinduzi wa Kamusi ya Kiswa¬hili-Kihispaniola kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Havana, Cuba.

Serikali ya Rais Samia imetam¬bua Kiswahili kama rasilimali muhimu ya kiutamaduni na kiu¬chumi, na UDSM inachangia kwa kuzalisha wataalamu wa Kiswa¬hili wanaoeneza lugha hii kwenye mataifa mbalimbali, hivyo kui¬marisha nafasi ya Tanzania kimataifa.


Lugha za kigeni na mchango wake katika ukuaji wa uchumi

UDSM inatoa mafunzo ya lugha mbalimbali za kigeni, ziki¬wemo Kichina na Kifaransa na sasa imeingia katika ushirikia¬no na Chuo cha Havana, Cuba kufundisha lugha ya Kihispan¬iola; Balozi za Angola na Brazil zinaisaidia UDSM kufundisha Kireno; Balozi za Kiarabu hasa Misri inasaidia UDSM kuweza kufundisha Kiarabu. Ufahamu wa lugha hizi za kimataifa una¬saidia sana kuwaandaa vijana kushiriki kwenye biashara, ajira na mahusiano ya kimataifa na hivyo kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa Taifa na kuongeza fursa za ajira kimataifa.


Matumaini makubwa siku za usoni

Kwa ujumla katika kipindi hiki cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan, Chuo Kikuu kime¬tekeleza miradi mingi muhimu sana ya kimkakati ambayo imeku¬wa nguzo muhimu katika kutimi¬za malengo na majukumu makuu ya UDSM yaani kutoa maarifa, kufanya tafiti na ubunifu na kutoa huduma kwa jamii.

Miradi hii, ambayo ama imete¬kelezwa kitaasisi au kupitia mfa¬nyakazi ikiwemo wanataaluma na watafiti imeleta tija kubwa kwa Chuo na Taifa kwa ujumla. Kupi¬tia miradi hii ajenda ya Mhe. Rais inayolenga kumletea maendeleo kila Mtanzania imezingatiwa kwa uzito, na ni chachu muhimu kwa mustakabali wa jamii na Taifa.