Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahojiano mtaalamu kimataifa wa tathmini ya ulinganifu wa mradi wa QUALITAN wa UNIDO, Ali Abbas Qazilbash (PhD) kuhusu MSMEs

Wataalamu kutoka maabara ya kemia wakishiriki mafunzo katika maabara ya TBS kuhusu uendeshaji wa mashine ya GCMS iliyonunuliwa kupitia mradi wa QUALITAN ili kuwezesha kupima uchafu wa kemikali kwenye bidhaa.

  1. Utangulizi wa mradi wa QUALITAN

Je, unaweza kutuelezea kuhusu mradi wa QUALITAN na malengo yake ya msingi?

Mradi wa QUALITAN ni mradi wa usaidizi wa kiufundi unaofadhiliwa na EU ambao lengo lake kuu ni kupanua wigo wa ufikiaji wa masoko kwa MSMEs kwa kuboresha ubora wa viwango, kupunguza gharama za upatikanaji wa vibali na kuimarisha ulinzi kwa walaji. Mradi huu unalenga katika uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini kulingana na mpango wa maboresho ya udhibiti wa Serikali na kuboresha mfumo wa ikolojia kwa ujasiriamali na ubunifu, hasa kwa MSMEs zinazoongozwa na wanawake na vijana.  

Mradi wa QUALITAN unafanya kazi ya kuimarisha uwezo wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na kufikia huduma za upimaji na urekebishaji, shughuli za mabadiliko ya kidijitali zinazohusiana na upimaji, mfumo wa taarifa za maabara (LIMS), ukuzaji viwango (QR code na webstore), ukaguzi na uthibitishaji wa mifumo ya usimamizi.


Kwa namna gani mradi unalenga kusaidia MSMEs Tanzania?

Mradi wa QUALITAN unalenga katika kuimarisha uwezo wa TBS, ambapo msaada utatolewa kwa MSMEs ili kuzingatia viwango, kupata huduma za upimaji, kupunguza gharama za upatikanaji wa vibali iwe katika masuala ya fedha au muda na kuwezesha upatikanaji wa masoko na biashara za nje ya mipaka.    

Zaidi ya hayo, kupitia juhudi za ushirikiano kati ya TBS na SIDO, mradi wa QUALITAN uliwezesha kuandaa mkakati wa kushughulikia mahitaji ya MSMEs kuhusu viwango vya ubora, usalama wa chakula na mahitaji ya soko. Hii ni pamoja na kuandaa mwongozo wa mafunzo ya pamoja katika masuala husika na mafunzo kwa wakufunzi kutoka SIDO na TBS ili kutoa mafunzo katika mikoa 10 nchini yanayolenga MSMEs 1000.


Changamoto zinazowakabili MSMEs

Je, ni changamoto gani zinawakabili MSMEs nchini katika suala la uzingatiaji wa ubora na viwango?

MSMEs wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo vifaa duni vya uzalishaji, miundombinu duni, mitaji duni ya kusaidia kukuza shughuli zao, usaidizi wa kitaasisi na kisheria usioratibiwa, upatikanaji duni wa masoko na ucheleweshaji wa malipo hasa katika utoaji wa huduma za umma.  

Je, mradi wa QUALITAN unashughulikiaje changamoto hizi?

Mradi wa QUALITAN unashughulikia changamoto zinazowakabili MSMEs wa Kitanzania katika uzingatiaji wa ubora na viwango kwa kuboresha uwazi katika udhibiti kupitia mifumo ya kidijitali, kupunguza gharama za upatikanaji wa vibali na kuboresha miundombinu ya TEHAMA, kuongeza uwezo wa kitaasisi kuwa na ufanisi katika ukaguzi na kusaidia kwa njia isiyo ya moja kwa moja ukuzaji wa ujuzi kupitia zana za kisasa.

TBS na SIDO zinashirikiana ili kuongeza usaidizi kwa MSMEs kupitia mkakati mahususi unaojumuisha mafunzo ya wakufunzi kutoka SIDO na TBS ili kutoa programu jumuishi ya mafunzo na kuandaa mwongozo kuhusu viwango vya ubora, usalama wa chakula na mbinu za kufikia masoko. Utekelezaji wa vipindi vya mafunzo kwa MSMEs, kulingana na mpango wa mafunzo wa SIDO unalenga kufikia hadi MSMEs 1000.

Jitihada hizi zinalenga kutengeneza mazingira bora ya biashara, kuwezesha MSMEs kufikia viwango kwa ufanisi zaidi na kushindana vyema katika masoko ya kikanda na kimataifa.


3. Umuhimu wa tathmini ya ulinganifu

Kwa nini tathmini ya ulinganifu ni muhimu kwa MSMEs, hasa wale wanaotaka kuingia katika masoko ya kimataifa?

Tathmini ya ulinganifu inaongeza thamani ya viwango na kuongeza imani kwa wanunuzi, watumiaji na wadhibiti kwamba bidhaa zinakidhi viwango vinavyotakiwa. Vipengele vya tathmini ya ulinganifu ni pamoja na ukaguzi, upimaji na uthibitishaji unaotumika katika nyanja zote za uchunguzi, uvumbuzi, mchakato wa uboreshaji, tija, ukuzaji wa uzalishaji wa bidhaa na mengine mengi.

Wataalamu kutoka Maabara ya Kemia ya Chakula ya TBS wakiwa katika ziara ya mafunzo katika Taasisi ya Taifa ya Vipimo ya Afrika Kusini (NMISA) kama sehemu ya shughuli za kujanga uwezo zinazofadhiliwa na mradi wa QUALITAN.


4. Nafasi ya UNIDO katika maendeleo ya MSME

Je, UNIDO inasaidia vipi maendeleo ya MSME duniani, na ni mikakati gani mahususi inayoitekeleza Tanzania?

UNIDO inasaidia maendeleo ya MSME duniani kwa kutoa usaidizi wa kiufundi, kujenga uwezo na kukuza ujasiriamali na upatikanaji wa fedha. Nchini Tanzania, UNIDO inatekeleza mikakati inayolenga sekta kama vile biashara ya kilimo na nishati mbadala, inaboresha mifumo ya sera na kuimarisha uwezo wa kitaasisi ili kukuza mazingira ya kusaidia ukuaji na uendelevu wa MSME. Juhudi hizi ni pamoja na mradi wa Waste-to-Energy kupitia GEF, matumizi ya teknolojia ya WTE, hasa matumizi ya biomass na biogas, katika viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo. UNIDO pia inatekeleza Mradi wa Masuluhisho ya Nishati ya Kupikia chini ya Mpango wa CookFund unaofadhiliwa na EU kwa kuhimiza matumizi ya Ethanol kama mafuta safi na mbadala kwa kupikia. Juhudi hizi zinalenga kuongeza ushindani, ubunifu na maendeleo jumuishi ya viwanda, hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.


Je, ni ushirikiano gani umeanzishwa chini ya mradi wa QUALITAN kwa ajili ya kuimarisha ukuaji wa MSME?

Ushirikiano kati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) katika kuendeleza programu ya ushirikishaji wa MSMEs na mchango kutoka Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) na Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania. TCCIA).


5. Mafunzo na kujenga uwezo

Je, ni aina gani ya programu za mafunzo na kujenga uwezo ambazo mradi wa QUALITAN unazitoa kwa MSMEs?

Mahitaji yanayozingatia viwango vya ubora, usalama wa chakula na mahitaji ya soko katika kushughulikia masuala yanayohusu mchakato wa uzalishaji, thamani ya bidhaa na upatikanaji wa masoko ya kikanda na kimataifa. Hizi ni pamoja na kanuni za usindikaji wa chakula, viwango na ubora wa bidhaa, ufungashaji na uwekaji lebo, urasimishaji wa biashara na uuzaji.


Ni jinsi gani MSMEs wanaweza kujiunga na programu hizo za mafunzo na watarajie faida gani katika shughuli zao?

Kwa kutumia wakufunzi walioandaliwa kupitia mafunzo ya wakufunzi (ToT) yaliyowezeshwa na mshauri wa MSMEs na wataalam wa TBS na SIDO, wakufunzi hawa watatoa mafunzo kwa MSMEs 1000 katika mikoa 10 ikijumuisha Dar es Salaam, Tanga, Singida, Ruvuma, Mwanza, Geita, Shinyanga (Kahama), Kilimanjaro, Kagera na Kigoma na wilaya 40 kati ya Agosti na Septemba 2024. Minyororo sita ya thamani ya mazao ya chakula italengwa katika mafunzo hayo ambayo ni mchele, asali, viungo, unga, samaki na mazao ya samaki na mafuta ya kula. Nyenzo za mafunzo na miongozo iliyoandaliwa na wataalam na kuthibitishwa kupitia tathmini ya mahitaji ya mafunzo na ToT itatumika kuwezesha vipindi vya mafunzo hayo.  

MSMEs watawezeshwa kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango na ubora kwa bei pinzani na kuruhusu ufikiaji wa masoko ya kikanda na kimataifa.


6. Uboreshaji wa miundombinu ya ubora

Ni hatua gani zinachukuliwa kuboresha miundombinu ya kitaifa ya ubora nchini?

UNIDO, kupitia mradi wa QUALITAN, imeshughulikia mapungufu ya miundombinu ya ubora nchini kwa kutumia kielelezo cha QI4SD ilichotengeneza ili kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa. Mradi pia uliboresha huduma za tathmini ya ulinganifu za TBS ambazo zingewezesha upatikanaji kwa urahisi wa huduma zinazohitajika kama uthibitisho wa bidhaa za Tanzania zilizothibitishwa kuwa salama kwa matumizi ya binadamu na zinazozingatia kanuni za usafi na usafi wa mazingira (SPS).

Je, maboresha haya yanatafsiriwa vipi kuwa fursa bora kwa MSMEs?

Maboresho ya miundombinu ya kitaifa ya ubora nchini yameongeza fursa kwa MSMEs kwa kufungua masoko mapya kwa njia ya ithibati bora na viwango vya kimataifa, kupunguza gharama za kufuata sheria na kanuni na kuongeza imani ya watumiaji katika bidhaa zao. Mifumo ya udhibiti iliyorahisishwa na huduma za usaidizi wa kiufundi husaidia MSME kufikia viwango kwa ufanisi zaidi, huku sheria mpya ikipunguza mizigo ya kiutawala na kuongeza uwazi. Maboresho haya yanazipa MSMEs nguvu ya ushindani, kuwezesha ukuaji na upanuzi wa masoko.  


7. Matokeo ya muda mrefu na endelevu

Ni kwa jinsi gani mradi wa QUALITAN unahakikisha uendelevu wa mikakati yake kwa MSMEs?

Kwa njia za kutoa mafunzo na kuhakikisha umiliki na uendelevu, mikakati hii iliundwa kuhusisha utaalamu kutoka TBS na SIDO kwa kushirikisha mashirika ya sekta binafsi (PSOs). Zana za mafunzo na wakufunzi zilizolenga MSMEs (TBS 10 na SIDO 10) zimeundwa ili kuwezesha kutoa mafunzo kama hayo katika muda wote wa uhai wa mradi. Mafunzo haya pia yameunganishwa katika mipango ya mafunzo ya SIDO kwa mwaka wa utekelezaji 2024.


Ni matokeo gani ya muda mrefu mnayoyaona katika sekta ya MSME nchini kutokana na mradi huo?

MSMEs zitakuwa na ushindani na hivyo kufikia masoko ya kikanda na kimataifa na hatimaye kuboresha hali zao kijamii na kiuchumi.


8. Ushauri kwa MSMEs

Ni ushauri gani unawapa MSMEs wa Tanzania kwa ajili kuboresha viwango vyao vya ubora na kupanua wigo wa masoko?

MSMEs zinapaswa kuelewa na kufikia viwango vya ubora vya kitaifa na kimataifa vinavyohusiana na sekta hiyo na pia kuanzisha mifumo thabiti ya kutoa bidhaa za ubora wa juu kila mara. Zinapaswa kutumia zana za dijitali kwa ajili ya kuhakikisha zinazalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu mara kwa mara. MSMEs pia zinapaswa kuwa na uelewa kuhusu mienendo ya sekta na mabadiliko ya udhibiti ili kuendelea kuwa washindani na kutengeneza utamaduni wa kuendeleza ubora na uvumbuzi.


Kwa jinsi gani MSMEs wanaweza kutumia rasilimali na usaidizi unaotolewa na mradi wa QUALITAN? 

Watumie miundombinu iliyoboreshwa ya ubora iliyopo TBS kupata huduma nafuu za tathmini ili kuthibitisha bidhaa kwa mahitaji ya soko. Vilevile, wajihusishe mara kwa mara na SIDO ili kupata maarifa mapya kuhusu taarifa mbalimbali zitakazowasaidia katika uendelezaji wa bidhaa zao na uongezaji thamani.


Mafanikio makubwa ya mradi

Kupitia mradi wa QUALITAN, TBS imenufaika na mafunzo ya watumishi 150 katika viwango mbalimbali, ukaguzi na upimaji, kupatiwa vifaa vya kisasa vya maabara 183 ili kurahisisha huduma za upimaji na kuandaa mipango ya biashara kwa kamati 101 za ufundi kwa ajili ya ukuzaji viwango na mipango ya biashara ya majaribio nane na maabara moja ya vipimo. QUALITAN pia itaboresha ufanisi wa TBS kupitia mageuzi ya kidijitali kwa kuunganisha miundombinu iliyopo ya TEHAMA na Mfumo wa Taarifa za Maabara (LIMS), msimbo wa QR na duka mtandao (webstore).

Mradi uliwezesha ushirikiano kati ya TBS na SIDO kupitia programu zao ili kuwawezesha MSMEs katika masuala yanayohusiana na ubora, usalama na uzingatiaji wa viwango. Hili litapelekea utayarishaji wa mwongozo wa mafunzo kwa MSMEs 1000 katika mikoa 10 kuhusu vipengele mbalimbali vya viwango, ubora, usalama, ufungashaji na kanuni bora za kimataifa.