Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EU, washirika wake watembelea Mwanza kuboresha uhusiano na kuzindua Mpango wa Maendeleo ya Uwekezaji Mijini

Mwanza. Ujumbe wa wakuu wa ushirikiano kutoka Umoja wa Ulaya (EU) pamoja na nchi wanachama wamekutana jijini Mwanza wiki hii kwa lengo la kutathimini uhusiano unaondelea kati ya EU na Tanzania na kujadili kuhusu njia za kuendeleza uhusiano huo, zinazolenga kuleta maendeleo endelevu mijini.

Ukiongozwa na Marc Stalmans, Mkuu wa Ushirikiano wa EU, ujumbe huo umejumuisha wawakilishi kutoka nchini za Ujerumani, Ubelgiji, Sweden, Ufaransa, Ireland, Denmark na Uholanzi. Ziara hiyo ya siku mbili jijini Mwanza imehusisha vikao kati wa ujumbe huo na uongozi wa mkoa, kutembelea miradi inayofadhiliwa na EU na kutekelezwa chini ya mpango wa nchi za Ulaya ambao unawaleta kwa pamoja Umoja wa Ulaya, nchi wanachama wake na mashirika ya maendeleo ili kutoa misaada kwa nchi washirika.

Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, ujumbe huo ulitembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda pamoja na mtambo wa kusafisha maji wa Butimba ambao ni moja kati uwekezaji wa kimkakati katika mradi wa maji na usafi wa mazingira wa Ziwa Viktoria awamu ya kwanza (LV WATSAN I), unaofadhiliwa na nchi za Ulaya.

Nchi za Ulaya zinajiandaa kufadhili awamu ya pili ya mradi huo kupitia mpango wa Miji Safi na ya kisasa (Green and Smart Cities SASA programme). Ukiwa na uwekezaji wa jumla ya Sh 813 bilioni (EUR 325 million) zikihusisha Sh 93 bilioni (EUR 75 million) kutoka mfuko wa EU na Sh 720 bilioni (EUR 250 million) ambao ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka kwa nchi wanachama, mpango huu umebuniwa ili kuboresha hali ya maisha ya mijini katika miji ya Mwanza, Tanga na Pemba.

SASA inaunga mkono juhudi za Tanzania za kukabiliana na ukuaji wa haraka wa miji kwa kuongeza ufaikiaji wa huduma za jamii, kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuongeza fursa za kiuchumi hususani kwa wanawake, vijana na jamii ambazo hazijafikiwa na huduma.

“Kupitia programu ya SASA, tunasaidia miji kuwa jumuishi, mistahimilivu pamoja na kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yatokanayo na ongezeko la watu.” Amesema Marc Stalmans, Mkuu wa Ushirikiano wa EU. “Ushirikiano huu sio tu kwa ajili ya miundombinu, bali pia kwa ajili utu, upatikanaji wa huduma na fursa kwa Watanzania.”

Aprili 10, ujumbe huo uliungana na Mkuu wa Mkoa kuzindua ofisi ya Programu ya SASA Mwanza. Ofisi hiyo itawaleta pamoja watekelezaji wa programu hiyo wakiwemo Wakala wa Ubelgiji wa ushirikiano wa kimataifa (Enabel), Shrika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).