Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Witts aeleza dhamira ya Coop Bank katika kuwafikia Watanzania wengi zaidi na huduma jumuishi

Mwenyekiti wa Bodi Coop Bank Tanzania Dk Josepth Witts.

Mwenyekiti wa Bodi ya Coop Bank Tanzania, Dk Joseph Witts amesisitiza dhamira ya benki hiyo katika kuimarisha ujumuishi wa kifedha nchini kufuatia uzinduzi wa tawi jipya la Morocco jijini Dar es Salaam.

Hafla ya uzinduzi watawi hilo iliyojaa shamrashamra, iliashiria hatua kubwa katika utekelezaji wa mikakati ya bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo kuhakikisha huduma bora za kifedha zinawafikia wananchi wengi zaidi, hususan katika maeneo yenye fursa kubwa za kiuchumi ambayo kwa muda mrefu yamekuwa hayapati huduma stahiki.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Dk Witts alieleza kuwa uzinduzi wa tawi hili si tukio la bahati mbaya, bali ni sehemu ya mpango kabambe wa kueneza huduma za Coop Bank Tanzania kwa Watanzania wengi zaidi.

Alibainisha kuwa kama wadau wa sekta ya ushirika (wanakope), benki hiyo inajisikia kuwa na wajibu mkubwa wa kuunga mkono jitihada za Serikali.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa huduma za kifedha hazibaki kwa watu wachache, bali ziwe nyenzo ya maendeleo kwa kila mwananchi, jambo ambalo litasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa letu kwa ujumla,” alisema Dk Witts.

Uamuzi wa kufungua tawi katika eneo la Morocco, Dar es Salaam, ulikuja baada ya upembuzi wa kina wa kimkakati. Dk Witts alifafanua kuwa Dar es Salaam ni kitovu cha biashara nchini na mchangiaji mkuu wa pato la taifa kupitia sekta mbalimbali.

Alitaja umuhimu wa Bandari ya Dar es Salaam na Soko la Kimataifa la Kariakoo, ambalo ni kiungo muhimu cha kibiashara kwa nchi za jirani na mataifa mengine ya nje

“Kwa uwepo wetu katika eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, tunalenga kuhudumia mfumo mzima wa kiuchumi wa jiji hili, kuanzia wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) hadi kampuni kubwa zinazochangia ukuaji wa viwanda,” alisema Dk Witts.

Na kuongeza kuwa, “Huu ulikuwa uamuzi wa makusudi wa bodi."

Uzinduzi wa tawi hilo unafanya idadi ya matawi ya benki hiyo kufikia sita nchini kote. Aidha, Dk Witts alisisitiza upekee wa Coop Bank kama taasisi pekee ya kifedha yenye makao yake makuu jijini Dodoma, hatua inayoiunganisha benki hiyo moja kwa moja na kitovu cha utawala wa nchi huku ikitanua mbawa zake katika miji ya kibiashara.

Kwa kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya jamii na biashara, Coop Bank inajipambanua kama kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.