Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Arusha, hema lililofungwa katika mnara wa saa 'clock tower' limenogesha shamrashamra hizo.
Tenti hilo la kulala watalii lililofungwa na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (Tawa) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa limekuwa kivutio kutokana na ukubwa, urembo na eneo lililowekwa.